Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Ufaransa: Nicolas Sarkozy kufikishwa mahakamani katika kesi ya Bygmalion

Mwezi mmoja na nusu baada ya kutiwa hatiani katika kesi nyingine, Nicolas Sarkozy anatarajia kuhukumiwa tena Alhamisi hii, Mei 20 katika mahakama ya mjini Paris.

Baada ya kutiwa hatiani mwezi Machi kwa ufisadi na ushawishi, Nicolas Sarkozy anatarajia kuhukumiwa kwa matumizi mabaya ya kampeni yake ya urais wa 2012.
Baada ya kutiwa hatiani mwezi Machi kwa ufisadi na ushawishi, Nicolas Sarkozy anatarajia kuhukumiwa kwa matumizi mabaya ya kampeni yake ya urais wa 2012. Anne-Christine Poujoulat AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani wa Ufaransa, anashukiwa kutumia akaunti zake za kampeni za uchaguzi wa urais wa mwaka 2012 kwa kiwango kilichozidi kisheria licha ya onyo kutoka kwa wahasibu.

Kesi hiyo, ambayo ilitarajiwa kuanza Machi 17, iliahirishwa kwa sababu ya kulazwa hospitalini kwa mmoja wa washtakiwa 14, aliyekuwa mgonjwa wa COVID-19.

Baada ya kuhukumiwa kifungo jela mwezi Machi - ikiwa ni hukumu ya kwanza kwa rais wa zamani - kwa ufisadi na ushawishi, Nicolas Sarkozy anatarajia kusikilizwa na majaji Alhamisi hii ya Mei 20 katika mahakama ya jijini Paris katika kesi ya akaunti ya kampeni inayojulikana kama Bygmalion.

Nani aliyepanga ufadhili wa juu katika kampeni ya Nicolas Sarkozy mwaka 2012. Nani aliyenufaika na ufadhili huo? Nani aliyekuwa na taarifa? Haya ndiyo maswali ambayo mahakama itapaswa kujibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.