Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ufaransa: Nicolas Sarkozy kusikilizwa katika kesi ya Bygmalion

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anasikilizwa leo Jumatano hii, Machi 17 katika kesi nyingine ya Bygmalion inayohusiana na matumizi ya fedha katika kampeni yake ya uchaguzi.

Sarkozi alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kifungo kingine cha miaka miwili ambacho hakimlazimu aende jela.
Sarkozi alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kifungo kingine cha miaka miwili ambacho hakimlazimu aende jela. © Studio graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Wiki mbili baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi na kutumia vibaya madaraka kwa maslahi ya kifedha, rais wa zamani sasa atalazimika kujieleza mwenyewe kuhusu matumizi ya fedha wakati wa kampeni yake ya uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2012.

Nicolas Sarkozy anashukiwa kuzidisha kiwango cha euro milioni 20 kinachoruhusiwa kisheria kwa kampeni za uchaguzi wa urais nchini Ufaransa.

Nicolas Sarkozy alijua kuwa matumizi yake ya kampeni yalizidi sana kiwango kilichowekwa kisheria? Hilo ndilo swali zima ambalo mahakama italazimika kujibu.

Nicolas Sarkozy, ambaye wakati huo alikuwa mgombea wa chama cha UMP alitumia milioni 43, wakati alitakiwa kutumia euro Milioni 22 na nusu kwa duru mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.