Pata taarifa kuu
UFARANSA-LIBYA-UCHUMI-SIASA

Ufadhili wa Libya: Nicolas Sarkozy akabiliwa na mashtaka ya njama ya uhalifu

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alishtakiwa Jumatatu baada ya siku nne za kusikilizwa kwa madai ya njama ya uhalifu katika uchunguzi unaohusiana na tuhuma kwaùba alitumia pesa kutoka Libya kufanya kampeni yake ya mwaka 2007, vyanzo kutoka Ofisi kuu ya Mashtaka vimebaini.

Nicolas Sarkozy.
Nicolas Sarkozy. REUTERS/Lionel Bonaventure
Matangazo ya kibiashara

Mashtaka mengine yanayomkabili Sakorzy ni ya ufisadi ambapo anadaiwa kunufaika na pesa za umma zilizoibwa na pia kupata ufadhili wa kampeni yake kinyume cha sheria

Kesi hii mpya ni ya nne katika fali hii ya Nicolas Sarkozy, ambaye anaendelea kusema kuwa hana hatia bali wanamfanyia "njama" baada ya mashtaka yaliyotolewa mwezi Machi 2018 kwa "ufisadi", "ubadhirifu wa fedha za umma" na "ufadhili haramu wa kampeni za uchaguzi".

Mwisho wa siku nne za kusikilizwa na kuhojiwa kwa zaidi ya saa arobaini kumalizika Jumatatu jioni, Nicolas Sarkozy alishtakiwa tena kwa kesi hii iliyochunguzwa na majaji Aude Buresi na Marc Sommerer, waliomrithi Serge Tournaire.

Mwishoni mwa mwezi Januari, ofisi ya mashtaka iliamua kuongeza muda wa uchunguzi wake. Ni ndani ya mfumo wa mashtaka haya ya ziada ambapo majaji wanaosimamia uchunguzi walimsikiliza tena Nicolas Sarkozy mwishoni mwa wiki iliyopita na Jumatatu pia.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Sakorzy ambaye alikuwa rais kati ya mwaka 2007 hadi 2012 amekanusha na kusema mashtaka hayo yamemchafulia jina bila hata ushahidi wowote. Waendesha mashtaka wanashuku Sakorzy na washirika wake walipokea mamilioni ya dola kutoka kwa serikali ya dikteta wa zamani wa Libya Muamar Gadhafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.