Pata taarifa kuu
UFARANSA-SARKOZY-HAKI

Kesi ya Bygmalion: Nicolas Sarkozy kujua hatima yake Alhamisi hii

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anatarajia kufahamishwa Alhamisi hii, Septemba 20 kama mahakama itathibitisha au la kuendelea kusikiliza kesi ya Bygmalion inayomkabili.

Nicolas Sarkozy, alipigwa picha Jumanne, Machi 21, 2018, akitoka nyumbani kwake.
Nicolas Sarkozy, alipigwa picha Jumanne, Machi 21, 2018, akitoka nyumbani kwake. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Hii ni hatua muhimu kwa hatima ya rais wa zamani wa Ufaransa ambaye alitumia njia zote zinazowezekana ili kuepuka kufikishwa mbele ya majaji.

Kesi ya Bygmalion inahusu kampeni za urais, ambapo inashtumiwa kuwa fedha nyingi zilitumiwa kiholela. Katika kampeni za uchaguzi wa urais wa mwaka 2012, Nicolas Sarkozy anashtumiwa kutumia kwa fujo fedha za serikali. Zaidi ya euro milioni 42 zilitumiwa katika kampeni zake, sawa na karibu mara mbili ya kiwango cha milioni 22.5 kilichowekwa kishria.

Kashfa hii iliibuka mnamo mwaka 2014 na ugunduzi wa mfumo mkubwa wa risiti zisizo halali kwa lengo la kuficha gharama kwa matumizi ya mikutano ya umma chini ya usimamizi wa kampuni ya Bygmalion.

Katika agizo lake, Jaji Serge Tournaire alibani kwamba mgombea Sarkozy, kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kampeni, alinufaika kwa wizi, lakini uchunguzi haukuweza kubainisha waliotoa maagizo kwa kufanyika wizi huo au aliyotoa taarifa ya mfumo huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.