Pata taarifa kuu
LIBYA-UFARANSA-SARKOZY-HAKI

Ufadhili wa Libya kwa kampeni za Sarkozy: Mahakama yachunguza uhalali wa uchunguzi

Kesi ya faragha ya Nicolas Sarkozy kuhusu ufadhili wa Libya kwa kampeni zake za uchaguzi inatarajiwa kusikilizwa mbele ya Mahakama ya Rufaa ya jijini Paris leo Jumatano.

Nicolas Sarkozy anashtumiwa kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Nicolas Sarkozy anashtumiwa kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Nicolas Sarkozy, rais wa zamani wa Ufaransa anatuhumiwa kufadhili sehemu ya kampeni yake ya uchaguzi ambao alishinda mwaka wa 2007 kwa fedha kutoka Libya.

Nicolas Sarkozy anatarajia kupinga uhalali wa uchunguzi wa mahakama katika kesi hii inayoibuka kwa mara nyingine.

Hii ni hatua muhimu ya kisheria katika kesi hii iliyofunguliwa miaka 7 iliyopita. Nicolas Sarkozy na mawaziri wake wa zamani, Claude Guéant, Éric Woerth na Brice Hortefeux watatoa maelezo mengi dhidi ya uchunguzi wa ufadhili wa Libya kwa kampeni yake katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2007.

Ikiwa kazi ya wachunguzi iliwezesha kukusanya idadi kubwa ya dalili tosha ambazo zinaunga mkono madai ya ufadhili wa Libya kwa kampeni za uchaguzi za Nicolas Sarkozy katika uchaguzi wa urais, hakuna ushahidi wowote wa sahihi uliopatikana.

Katika rufaa yake, Nicolas Sarkozy, aliyeshtakiwa kwa ufisadi wa kupita kiasi, ufadhili haramu wa kampeni, kutuma fedha za umma kutoka Libya kinyume cha sheria, kwanza anadai kinga yake ya urais iweze kutambuliwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili baada ya kuchaguliwa kuwa rais.

Nicolas Sarkozy anashtumiwa kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Mwaka 2013, Ufaransa ilianzisha uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba kampeni ya Sarkozy ilipokea mchango kutoka kwa hazina ya pesa haramu za Gaddafi.

Bw Sarkozy ameendelea kukanusha tuhuma hizo.

Tuhuma hizo zilitolewa na mfanyabiashara Mfaransa mwenye asili ya Lebanon Ziad Takieddine na baadhi ya maafisa wa zamani wa Gaddafi.

Novemba 2016, Ziad Takieddine aliambia kituo cha habari cha Mediapart kuwa kati ya 2006-2007, alikabidhi mikoba mitatu iliyojaa noti za euro 200 na 500 kwa Bw Sarkozy na mkuu wa watumishi wake Claude Guéant.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.