Pata taarifa kuu
LIBYA

Libya: Macron atambua "deni" la Ufaransa kwa Libya mwaka 2011

"Tunadaiwa na Libya, hilo liko wazi kabisa: muongo mmoja wa machafuko. "Maneno haya ya Emmanuel Macron, aliyoyaambia viongozi wapya wa Libya Jumanne Machi 23 katika Ikulu ya Elysee, yanasikika kama kukiri kosa.

Mohammed el-Menfi, rais wa Baraza la utawala la Libya, Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa, na Musa al-Koni, makamu wa rais wa Baraza la utawala la Libya, katika Ikulu ya Elysee Machi 23, 2021.
Mohammed el-Menfi, rais wa Baraza la utawala la Libya, Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa, na Musa al-Koni, makamu wa rais wa Baraza la utawala la Libya, katika Ikulu ya Elysee Machi 23, 2021. AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Kuingilia kati dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011, kulioungwa mkono wakati huo na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, hali ambayo ilisababisha athari kubwa katika Sahel, amesema rais Emmanuel Macron.

Kwa maneno haya, yaliyochukuwa sekunde sita, Emmanuel Macron kwa mara ya kwanza alitambua rasmi jukumu la Ufaransa katika shida ambazo zinaikumba Libya na sehemu ya Afrika kwa miaka kumi.

Wakuu wa nchi za Sahel wanalalamika mara kwa mara juu ya athari za uingiliaji wa nchi za Magharibi dhidi ya Muammar Gaddafi mnamo mwaka 2011: kuangushwa kwa utawala wa Gaddafi kulisababisha kukosa fedha kutoka Tripoli, lakini pia kulisababisha wapiganaji wenye silaha kukimbilia katika ukanda huo na kusababisha mdororo wa usalama. Hali ambayo ilisababisha " kuwasili kwa mamluki wa mataifa mbalimbali ", kama alivyosema Idriss Déby, rais wa Chad, akihojiwa na RFI Agosti 2020.

Kwa upande wake rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alibaini wakati huo kuwa uingiliaji kijeshi nchini Libya, kwa wito wa Nicolas Sarkozy, ilikuwa kosa kubwa kutoka kwa Nicolas Sarkozy.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.