Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

Libya: Waziri mkuu aliyechaguliwa atangaza mpango wa serikali ya Umoja

Mpango wa serikali umewasilishwa kwa Bunge la Libya, Waziri Mkuu mteule Abdoulhamid Dbeibeh, aliyechaguliwa mwezi uliopita kama sehemu ya mazungumzo kati ya wadau wote nchini Libya yaliyoandaliwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Waziri Mkuu mpya wa Libya, Abdul Hamid Mohammed Dbeibah, kwa mkutano kwa njia ya video huko Geneva mnamo Februari 3, 2021.
Waziri Mkuu mpya wa Libya, Abdul Hamid Mohammed Dbeibah, kwa mkutano kwa njia ya video huko Geneva mnamo Februari 3, 2021. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya mpito itakuwa na jukumu la kuchukua nafasi ya tawala mbili hasimu za Libya na kuongoza Libya kuelekea uchaguzi mnamo mwezi Desemba.

"Serikali hii itaundwa na watu kutoka makundi mbalimbali ambao wataiwakilisha Libya," Abdoulhamid Dbeibeh amesema katika mkutano na waandishi wa habari jijini Tripoli.

Waziri Mkuu mteule ameongeza kuwa amejaribu "kushirikisha pande zote" kati ya magharibi, mashariki na kusini mwa nchi.

Libya imeingia katika machafuko tangu mapinduzi ya mwaka 2011 ambayo yalimwondoa mamlakani dikteta wa zamani Muammar Gaddafi. Tangu mwaka 2014 nchi hiyo imeongozwa na serikali mbili zinazokinzana, mashariki na magharibi, zikiungwa mkono na wanamgambo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.