Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAQ-HOLLANDE-ULINZI

Rais wa Ufaransa ziarani nchini Iraq

Rais wa Ufaransa François Hollande amewasili nchini Iraq Jumatatu hii Januari 2 ambapo atawatembelea wanajeshi wa Ufaransa wanaoendesha operesheni nchini humo katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic State.

François Hollande atakuwa nchini Iraq ambapo Ufaransa iliungana na mataifa mengine katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic Satte, Jumatatu, Januari 2, 2016.
François Hollande atakuwa nchini Iraq ambapo Ufaransa iliungana na mataifa mengine katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic Satte, Jumatatu, Januari 2, 2016. REUTERS/Stephane De Sakutin
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa rais Hollande, ambaye si mgombea wa uchaguzi wa urais kwa muhula wa pili, amesema hii ni nafasi ya kuonyesha kwamba bado anaendelea na majukumu yake wakati ambapo kampeni ya uchaguzi wa 2017 zinatarajia kuanza.

François Hollande anaendelea na majukumu yake mpaka muda wake wa mwisho.

Nchini Iraq, askari 450 wa Ufaransa, wanaendesha operesheni dhidi ya kundi la Islamic State pembezoni mwa mkoa wa Mosul, lakini pia vikosi maalum vya nchi hiyo vinaendelea kuwapa mafunzo ya kijeshi askaeri wa Iraq, kwa kupambana dhidi ya makundi ya kigaidi, ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic Sate. Mbali na hayo Ufaransa ina ndege za kivita katika Falme za Kiarabu na nchini Jordan katika ujumbe wa hammal. Kwa jumlaUfaransa ina askari 1 200 wanaoshiriki operesheni mbalimbali katika ukanda huo chini ya amri ya Rais wa François Hollande.

Ziara hii pia ni namna ya kuonyesha uungwaji mkono kwa jeshi la Ufaransa, siku kadhaa baada ya kiongozi wa majeshi ya Ufaransa Pierre de kuomba kuongezwa kwa kiwango cha kutosha cha bajeti katika maswala ya ulinzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.