Pata taarifa kuu
UFARANSA

Watu wawili wapandishwa kizimbani nchini Ufaransa na kushtakiwa kwa ugaidi

Wanaume wawili wanaohusishwa kuwa na uhusiano na raia wa Ufaransa mwenye itikadi kali, Rachid Kassim, wameshtakiwa kwa makosa ya kujihusisha na makundi ya kigaidi, imesema taarifa ya mwendesha mashtaka wa jiji la Paris.

Rachid Kassim, gaidi raia wa Ufaransa anayetakiwa na nchi yake.
Rachid Kassim, gaidi raia wa Ufaransa anayetakiwa na nchi yake. Fuente: Video de propaganda del Estado Islámico.
Matangazo ya kibiashara

Wanaume hao wenye umri wa kati ya miaka 30 na 39, walikamatwa Ijumaa ya wiki iliyopita magharibi mwa mji wa Dole na Roanne, ambako ni mji alikozaliwa Kassim, raia aneytajwa na Serikali kuwa hatari zaidi na kinara wa kundi la Islamic State.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa na uhusiano na Rachid kabla hajaenda nchini Syria au Iraq mwezi May 2015.

Kassim mwenye umri wa miaka 29, anatuhumiwa kutumia programu ya simu aina ya telegram, kutoa maelekezo ya namna ya kutekeleza mashambulizi nchini Ufaransa akitokea kwenye ngome inayokaliwa na wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.

Mtu mmoja wa karibu na mmoja wa watuhumiwa ameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa, kati yao alikuwa na mawasiliano ya hivi karibuni na mtuhumiwa Rachid, kupitia program ya Telegram.

Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa mkubwa wa watuhumiwa hao, alichangia kwa sehemu kubwa kupandikisha itikadi kali kwa Kassim.

Kassim ambaye ameonekana mara kadhaa kwenye picha za video za kundi hilo akieneza propaganda na kuhimiza chuki na kutekelezwa kwa mauaji ya Polisi wanandoa waliouawa hivi karibuni jijini Paris, mwezi Juni pamoja na mauaji ya mchungaji kwenye mji wa Normandy mwezi Julai.

Kassim anadaiwa kuwa alikuwa kishawishi kikubwa cha wasichana watatu waliokamatwa hivi karibuni jijini Paris wakijaribu kutekeleza shambulio la kigaidi.

Kassim pia anadaiwa kuwa na mawasiliano na mmoja wa wanawake wenye msimamo mkali, ambaye alikamatwa September 8 na kushtakiwa kwa makosa ya kupanga njama za kutekeleza shambulio la kigaidi katikati mwa jiji la Paris kwenye kanisa la Notre Dame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.