Pata taarifa kuu
KENYA

Mawasiliano yakwamisha kuanza kwa kesi ya ugaidi nchini Kenya

Changamoto ya mawasiliano imechelewesha kuendelea kwa kesi ya ugaidi dhidi ya washukiwa watatu wanaotuhumiwa, kuwapa hifadhi wanawake watatu walioshambulia kituo Kikuu cha Polisi mjini Mombasa Pwani ya Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wanawake watatu wakiwa Mahakamani mjini Mombasa wanashukiwa kuwapa hifadhi wanawake watatu walioshambulia kituo cha Polisi mjini Mombasa
Wanawake watatu wakiwa Mahakamani mjini Mombasa wanashukiwa kuwapa hifadhi wanawake watatu walioshambulia kituo cha Polisi mjini Mombasa LABAN WALLOGA | NATION MEDIA GROUP
Matangazo ya kibiashara

Imebainika kuwa washukiwa hao ni raia wa kigeni kutoka nchini Somalia.

Mmoja wa washukiwa hao Shukri Haji, ambaye ni kiziwi ameiambia Mahakama kuwa alikuwa haelewi kile ambacho mtafsiri wa lugha ya ishara alikuwa anamwambia.

Jaji Emmanuel Mutunga ameagiza kuwa washukiwa hao wote ambao hawawezi kuzungumza Kiswahili au Kiingereza, wazuiliwe kwa siku tano zaidi ili wapimwe akili kufahamu ikiwa wana uwezo wa kuwasiliana au la.

Polisi wanasema wanawake watatu waliokuwa wamejihami na mabomu na kisu na kuvamia kituo cha polisi kwa madai kuwa walikuwa wamekwenda kuripoti kuibiwa simu na kupigwa risasi na polisi hadi kuuawa baada ya kubainika kuwa ni magaidi, walikuwa ni raia wa Kenya.

Aidha, ripoti zinasema wanawake hao walikuwa ni wafuasi wa kund la Islamic State.

Maafisa wa ujasusi nchini Kenya wanashuku kuwa zaidi ya wanaume na wanawake 100 kutoka nchini humo wamekwenda kupata mafunzo ya kigaidi kutoka kundi la Islamic State nchini Libya na Syria.

Tangu serikali ya Kenya ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia mwaka 2012, kupambana na magaidi wa Al Shabab, imeendelea kukabiliana na tishio la kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.