Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI

Kijana mmoja akamatwa Paris kwa tuhuma za ugaidi

Katika mazingira ya tishio la kigaidi ya "kiwango cha juu" muda mfupi baada ya kuvunjwa kwa kundi la wanajihadi wanawake waliokua waliandaa mashambulizi nchini Ufaransa, kijana mwengine mwenye umri wa miaka kumi na tano alikamatwa Jumamosi Septemba 10 katika mji wa Paris.

Askari polisi wazidisha ulinzi katika maeneo mbalimbali mjini Paris Julai 20, 2016.
Askari polisi wazidisha ulinzi katika maeneo mbalimbali mjini Paris Julai 20, 2016. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Kijana huyu anatuhumiwa kuwa alikua tayari kutekeleza mashambulizi katika ardhi ya Ufaransa. Hivi sasa kijana huyo amewekwa kizuizini na kuhojiwa na polisi, wasifu wake unazusha swali la ugaidi ambapo watu wanaotekeleza mashambulizi haya wengi ni wenye umri mdogo. Na kati yao kuna wasichana wadogo.

Kijana huyo aliyekamatwa katika mtaa wa 12 mjini Paris anajulikana kwa polisi. Kufuatia msako wa viongozi tawala uliyofanyika nyumbani kwake miezi sita iliyopita, aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi.

Alikua amepanga kutekeleza mashambulizi katika maeneo wanakokaa watu wengi mjini Paris. Kwa mujibu wa vyanzo vya mahakama, kijana huyo alikua na uhusiano na Rashid K., mwenye umri wa miaka 29, mwanachama wa kundi la la Islamic State, ambaye alikua "akimuongoza" mmoja wa wasichana watatu waliokamatwa hivi karibuni.

Kijana huyo Mfaransa, anaonekana mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii, ambako amekua mara kwa mara akitoa wito kwa mauaji. nasemekana kuwa alifuata itikadi za Adel K na Abdel P., wauaji wa kasisi Jacques Hamel Julai 26 katika mji wa Saint-Etienne-du-Rouvray (Seine-Maritime).

Watoto hawa, ambao wakati mwengine ni chanzo cha miradi ya kigaidi, kama katika mpango wa kielimu ambayo imeanza kufanikiwa, sio mambo ya kupuuzia, kwa mujibu wa mwendesha mashitaka, Francois Molins. Katika mahojiano na gazeti la kila siku la Le Monde, ameshuhudia kesi nyingi ambapo wasichana wanahusika. Wana uhusiano wa kutisha, hasa pamoja na watu vigogo.

Mwezi uliopita, kijana mwenye umri wa miaka 16 alishtakiwa kwa kutangaza kwenye kifaa cha ujumbe kiliyolindwa, nia yake ya kutekeleza mashambulizi.

Mwezi Machi, wasichana wawili wenye umri mdogo waliwekwa jela baada ya kutangaza kupitia Facebook mashambulizi dhidi ya ukumbi wa tamasha mjini Parisi.

Mwaka mmoja uliyopita, wasichana watatu wenye umri wa miaka 15 hadi 17 walkua na mpango mbaya wa kutaka kuua Wayahudi katika mji wa Lyon.

Hadi sasa, watoto 35 wamefanyiwa uchunguzi na mahakama. Kati ya yao, kumi na wawili ni wasichana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.