Pata taarifa kuu
UFARANSA

Polisi Ufaransa inawahoji wanawake 3 kwa tuhuma za ugaidi

Polisi nchini Ufaransa inachunguza gari lililokuwa na mitungi sita ya gesi jijini Paris ambapo inawashikilia wanawake watatu wanaotuhumiwa kuwa walipanga njama za kutekeleza shambulio, ambapo mmoja kati yao alipigwa risasi na Polisi.

Polisi wakionekana kupiga doria kwenye eneo la Notre Dame katikati ya jiji la Paris.
Polisi wakionekana kupiga doria kwenye eneo la Notre Dame katikati ya jiji la Paris. REUTERS/Charles Platiau/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kwenye tukio hilo, pia Polisi mmoja alijeruhiwa kwa kisu wakati wa kuwakamata watuhumiwa hao, ambao wametajwa kuwa na umri wa miaka 39, 23 na 19, ambao walikuwa wanapanga njama za kutekeleza shambulio la kigaidi, alisema waziri wa mambo ya ndani ya nchi ya Ufaransa, Bernard Cazeneuve.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wanaohusika kwenye uchunguzi huo, ameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa, msichana aliyepigwa risasi alikuwa ni mtoto wa mmoja wa watuhumiwa hao ambaye aliapa kuwa mtiifu kwa kundi la kiislamu la Islamic State.

Mmoja wa raia aliowaona wanawake hao kabla ya kukamatwa kwenye eneo la Boussy-Saint-Antoine, kusini mwa jiji la Paris, amesema wanawake hao walikuwa na hofu muda mwingi na walikuwa wakitazamatazama pande walizokuwa wakitokea.

Shuhudia huyo amesema kuwa, baada ya Polisi kumkaribia mmoja wa wanawake, alitoa kisu na kumchoma askari sehemu ya tumbo.

Watu wanne, kaka wawili na wachumba zao, walikuwa tayari wanashikiliwa kwenye gari, ambao walipatikana mita chache kutoka kwenye eneo la tukio la kanisa maarufu la Notre Dame katikati mwa jiji la Paris.

Watu wawili ambao ni mtu na mke wake, wanashikiliwa na Polisi toka Jumanne ya wiki iliyopita, ambapo walikuwa wakifahamika na Polisi kwakuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi.

Mamlaka nchini Ufaransa zinasema kuwa, zinawasaka watoto wawili wa wamiliki wa gari aina ya Peugeot 607 lililokuwa limetelekezwa siku ya Jumapili jirani na kanisa la Notre Dame, eneo ambalo huvutia mamilioni ya watalii kila mwaka.

Katika hatua nyingine, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amelaani jaribio la kombora la Nyuklia lililofanywa na Serikali ya Korea Kaskazini, akisema jaribio hilo ni kinyume na mkataba wa kimataifa unaokataza majaribio ya silaha kali, na ni wazi taifa hilo limeendelea kukaidi onyo la jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.