Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-UJERUMANI

Shambulizi la mjni Berlin: mtuhumiwa aliyeuawa nchini Italia alipita Ufaransa

Mtuhumiwa mkuu katika shambulio la mjini Berlin, nchini Ujerumani alionekana nchini Ufaransa, kwenye kituo cha treni cha Lyon Part-Dieu, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama. Inaaminika kuwa alipita kwenye mipaka miwili na kuingia katika nchi tatu.

Mtuhumiwa mkuu katika shambulio mjini Berlin (picha iliyopigwa Disemba 19) alionekana nchini Ufaransa, kwenye kituo cha treni cha Lyon Part-Dieu, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.
Mtuhumiwa mkuu katika shambulio mjini Berlin (picha iliyopigwa Disemba 19) alionekana nchini Ufaransa, kwenye kituo cha treni cha Lyon Part-Dieu, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama. REUTERS/Pawel Kopczynski
Matangazo ya kibiashara

Mtuhumiwa kutoka Tunisia Anis Amri alionekana kwenye kituo treni cha Lyon Part-Dieu, kwenye picha za video zilizonaswa na kamera za ulinzi Alhamisi Desemba 22 mchana, siku moja baada ya kutolewa hati ya Ulaya ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Katika video hizo, mtuhumiwa anaonekana akijiandaa kupanda treni kuelekea katika mji wa Chambery. Hata hivyo hakuendelea hadi Chambery, lakini alipofika katika mji wa Turin aliondoka katika treni na kupanda nyingine kuelekea Sesto San Giovanni, wilaya inayopatikana kaskazini mwa mji wa Milan.

Tiketi mbili za treni katika mkoba

Nchini Italia, mtuhumiwa aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi ya Italia baada ya operesheni ya ukaguzi wa vitambulisho, na tiketi mbili za treni zilikutwa katika mkoba wake. Angalau moja ya tiketi hizo ambayo ilikua kwenda Lyon-Chambéry-Milan kupitia Turin, ilinunuliwa fedha taslimu kwenye kituo cha treni cha Lyon Part-Dieu, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi. Lakini haijulikani ni jinsi gani tiketi hizo zilinunuliwa, na kama kulikua na mtu aliyehusika na kukunua tiketi hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.