Pata taarifa kuu

Mtuhumiwa mkuu katika shambulio la mjini Berlin auawa nchini Italia

Baada ya siku nne polisi ya Ulaya ikimtafuta mtuhumiwa wa shambulio la mjini Berlin, hatimaye Anis Amri , raia wa Tunisia mwenye umri wa miaka 24, aliuawa usiku wa kuamkia Ijumaa hii na polisi katika mji wa Milan, nchini Italia.Taarifa ambayo imethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia.

Polisi wakipiga doria katika ufunguzi wa soko la bidhaa za Krismasi karibu na kanisa la Kaiser Wilhelm Gedaechtniskirche mjini Berlin, Desemba 22, 2016.
Polisi wakipiga doria katika ufunguzi wa soko la bidhaa za Krismasi karibu na kanisa la Kaiser Wilhelm Gedaechtniskirche mjini Berlin, Desemba 22, 2016. CLEMENS BILAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Anis Amri amekua akitafuta na polisi ya Ulaya tangu kutokea kwa shambulizi la mjini Berlin lililogharimu maisha ya watu 12, na wengine kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa vyombo kadhaa vya habari vya Italia, vinavyozungumzi taarifa ya polisi, Anis Amri alikamatwa akiwa katika gari ndogo mapema Alfajiri kwenye saa 9, wakati wa zoezi la kukagua vitambulisho vya uraia.

Mwandishi RFI katika mji wa Rome Anne Le Nir, anaarifu kuwa Anis Amri alijaribu kutoa ndani ya mkoba wake bunduki ndogo aina ya bastola 22. Inasadikiwa kuwa alirusha risasi dhidi ya askari polisi wawili na kumjeruhi mmoja wao kwenye bega, kabla ya kupiga kelelea akisema "Allah Akbar! "

Katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Marco Minniti, alisema kuwa Anis Amri aliye uawa, bila shaka" alikua mtuhumiwa mkuu wa shambulizi la mjini Berlin, lililosababisha vifo vya watu 12na hamsini waliojeruhiwa kwenye soko la bidhaa za Krismasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.