Pata taarifa kuu
UJERUMANI-SAMBULIZI-USALAMA

Polisi ya Ujerumani yamsaka raia wa Tunisia

Polisi nchini Ujerumani wanamsaka raia wa Tunisia anayefahamika kwa jina la Anis A, anayeshukiwa kuwagonga watu waliokuwa wanafanya manunuzi katika soko la kuuza bidhaa vya sikukukuu ya Krismasi mjini Berlin siku ya Jumatatu usiku.

Eneo la shambulizi la Novemba 19, 2016 katika mji wa Berlin, siku moja baada ya tukio hilo.
Eneo la shambulizi la Novemba 19, 2016 katika mji wa Berlin, siku moja baada ya tukio hilo. REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Islamic State lilidai kutekeleza shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 12 na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa.

Ripoti zinasema kuwa mshukiwa huyo ni mkimbizi na alipewa hifadhi nchini humo mwaka uliopita.

Jumanne wiki hii, kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alisema kuwa bado atashangaa iwapo mtu aliyehusika na shambulizi hilo atakua ni mkimbizi aliyepewa hifadhi ya ukimbi nchini Ujerumani.

Picha ya kijana kutoka Tunisia imesambazwa nchini Ujerumani

Vyeti vilivyopatikana katika lori ni vile vya mtu aliyezaliwa mwaka 1992 katika mji wa Tataouine, ambaye anaitwa kwa jina Anis A., anayeonekana kuwa ni mtu aliyeomba hifadhi ya ukimbizi miezi michache iliyopita. Kijana huyo aliyeorodheshwa kwa majina tofauti kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani, alionekana kuwa ni mmoja wa watu wanaochukuliwa kuwa hatari nchini Ujerumani.

Hata hivyo katika uchunguzi unaoendelea kuhusu mazingira ya mashambulizi hayo, lori lililotumiwa kwa shambulizi hilo liiliibiwa kutoka kwa dereva wa Poland wakati alipokua aipumzika. Dereva huyu alipatikana baada ya shambulio hilo, aliuawa kwa risasi kwenye kiti cha abiria katika lori hilo. Mwili wake ulikutwa na majeraha ya kisu.

Kitita cha Euro 100,000 kimetolewa kwa yeyote yule atakayemkamata au kuonyesha alipo kijana huyo kutoka Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.