Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UFARANSA-USALAMA-UGAIDI

Mashambulizi ya Paris: Salah Abdeslam akamatwa Brussels

Salah Abdeslam, mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, amekamatwa Ijumaa hii Machi 18 katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, vyanzo vya polisi vikinukuliwa na shirika la habari la Ufaransa la AFP, vimesema.

Operesheni kabambe ya polisi ilianzishwa Ijumaa, Machi 18, 2016 katika wilaya ya Molenbeek, mjini Brussels.
Operesheni kabambe ya polisi ilianzishwa Ijumaa, Machi 18, 2016 katika wilaya ya Molenbeek, mjini Brussels. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Alama za vidole vyake zimepatikana katika ghorofa iliofanyia msako na vikosi vya polisi vya Ubelgiji na Ufaransa Jumanne Machi 15.

Salah Abdeslam anakamatwa baada ya kusakwa kwa kipindi cha miezi minne. mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 katika mji wa Paris amekamatwa jumaa hii Machi 18 katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels wakati wa operesheni kababme ya polisi. Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi vikinukuliwa na shirika la habari la la Ufaransa la AFP, mtu mmoja amjeruhiwa.

Operesheni ya kumkamata Abdeslam Salah imeanzishwa baada ya msako wa Machi 15 katika eneo la Forest, kitongoji cha Brussels, ulioendeshwa na vikosi vya polisi vya Ubelgiji na Ufaransa. Wakati wa operesheni hii, maafisa wa polisi wanne wamejeruhiwa, wakati ambapo mtu mmoja ameuawa na vikosi vya usalama. Inasadikiwa kuwa ni mmoja wa watuhumiwa waliohifadhi vifaa vya mashambulizi. "Mohamed BelkaΓ―d alieuawa katika eneo la Forest Jumanne wiki hiini ni mmoja wa washirika wa Salah Abdeslam. Alitumia jina la uongo la Samir Bouzid. Huu ni mmoja watuhumiwa waliohifadhi vifaa vilivyotumiwa katika mashambulizi ya Paris, " shirika la utangazaji la RTBF limeangika katika tovuti yake.

Vinasaba vya damu vya Abdeslam vilipatikana katika mabaki

Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imethibitisha Ijumaa hii mchana kwamba alama mbili za Salah Abdeslam ziligunduliwa katika nyumba moja. Kuna kwanza vinasaba vya damu lakini pia alama ya vidole. alama ya vidole imepatikana kwenye kioo kichafu kilichotokana na risasi au urushianaji risasi mara tatu uliotokea kati ya kuwasili kwa wachunguzi kwa ajili ya msako walidhani kuendesha kila mara na wakati ambapo mtu anayeshukiwa kuwa mwanajihadi wa mwisho alipigwa risasi na askari polisi mzoefu.

Salah Abdeslam anaweza kuwa mmoja wa watu wawili ambao walikimbia wakipitia kwenye paa wakati wa mchana kabla ya kutoweka, na tangu wakati huo walianza kusakwa na polisi nzima ya Ubelgiji na Ufaransa. Itafahamika kwamba Ofisi ya mashtaka imekataa kutoa maelezo yoyote yanayohusiana na taarifa hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.