Pata taarifa kuu
UBELGIJI-USALAMA-UGAIDI

Ubelgiji: askari polisi washambuliwa kwa risasi Brussels

Askari polisi wa Ufaransa wameshiriki Jumanne hii katika msako mjini Brussels, nchini Ubelgiji katika sehemu ya uchunguzi wa mashambulizi yaliotokea mjini Paris, wakati ambapo watu wenye silaha walishambulia kwa risasi vikosi vya Usalama.

Askari polisi wakiwa karibuna eneo kulikotokea shambulizi la risasi katika wilaya ya Forest, karibu na mji wa Brussels, Machi 15, 2016.
Askari polisi wakiwa karibuna eneo kulikotokea shambulizi la risasi katika wilaya ya Forest, karibu na mji wa Brussels, Machi 15, 2016. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Hayo ameyasema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan.

"Kama sehemu ya msako, timu inayoundwa na askari polisi wa Ubelgiji na Ufaransa wameingilia kati na kuzima shambulio hilo, lakini niko makini kuhusu mazingira ya shambulio hilo. Makini kwa sababu kuna hatua inayoendelea na sintoelezea chochote ispokua kuthibitisha hali imedhibitiwa," amesema wakati wa ziara yake nchini Cote d'Ivoire, baada ya shambulizi la kijihadi lililowaua watu18 Jumapili hii katika mji wa mapumziko wa Grand-Bassam. Operesheni kuu ya polisi kwa sasa inaendelea nchini Ubelgiji.

Operesheni ya polisi ilioendeshwa Jumanne hii katika mji wa Brussels haikua inamlenga Salah Abdeslam, mhusika mkuu wa mashambulizi ya mjini Paris ya mwezi Novemba, lakini watu walio karibu na watuhumiwa nchini Ubelgiji walio husika katikamashambulizi hayo, chanzo cha polisi kimeeleza.

"Operesheni hii hakuwa inamlenga Salah Abdeslam lakini watu walio karibu na watuhumiwa 11, raia wa Ubelgiji, waliohusika katika mashambulizi ya mjini Paris," chanzo hicho kimesema. taarifa hii imethibitishwa kwa Shirika la habari la Ufaransa la AFP na chanzo kilio karibu na kesi hii. Abdeslam Salah, mwenye umri wa miaka 26, anayetuhumiwa kuhusika katika moja ya mambo muhimu ya mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu 130, hajulikani aliko tangu wakati huo.

Itafahamika kwamba vikosi vya maafisa wa usalama nchini Ubelgiji vimekua vikiwasaka watu wawili baada ya maafisa wa polisi kufyatuliwa risasi katika oparesheni dhidi ya ugaidi katika mji mkuu wa Brussels.

Kisa hicho kilitokea katika makaazi ya kusini ya ForestMaafisa watatu walijeruhiwa huku mmoja wao akijeruhiwa vibaya.

Mwendesha mashtaka amesema kuwa uvamizi huo unahusishwa na shambulio la Paris ambalo liliwaua watu 130 mwezi Novemba mjini Paris.

Maafisa wa polisi wa Ubelgiji wamekuwa wakijaribu kuwasaka wapiganaji kutoka kwa kundi la Islamic State.

Askari polisi wanne wamejeruhiwa katika operesheni hiyo uya ploisi. Watatu wamejeruhiwa wakati wa msako uliokua ukifanyika katika wilaya ya Forest mjini Brussels, na askari polisi wanne amejeruhiwa kwa risasi katika operesheni iliofuata katika kata moja ya wilaya hiyo, amesema Eric Van der Sypt, msemaji wa Ofisi ya mashitaka. Vyombo vya habari vimekua vikiarifu mpaka sasa kwamba askari polisi watatu ndio wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyorushwa hewani kwenye shirika la utangazaji la RTBF nchini Ubelgiji, mshukiwa moja ameuawa na wengine wasiofahamika idadi wametoweka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.