Pata taarifa kuu
UFARANSA-HALI YA TAHADHARI

Ufaransa: muda wa hali ya tahadhari waongezwa

Hatari ya tahadhari nchini Ufaransa imeongezwa muda wa miezi mitatu kuanzia Februari 26, mpaka Mei 26. Uamuzi huo ulmepitishwa Jumanne Februari 16 na Bunge, ambapo kura 212 dhidi 31 zilipigwa, na 3 hazikuonyesha msimamo wowote, lakini hali hii inaibua mengi katika kambi ya upinzani.

Ufaransa inaishi chini ya utawala wa hali ya tahadhari tangu Novemba 13, 2015.
Ufaransa inaishi chini ya utawala wa hali ya tahadhari tangu Novemba 13, 2015. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Serikali, kwa upande wake, inasisitiza kuwa tishio la kigaidi ni liko katika "kiwango cha juu zaidi ya kile kinachoshuhudiwa."

Zaidi ya taratibu 500 zilizofunguliwa kufuatia upekuzi zimeruhusu hali ya tahadhari, baadhi tu taratibu hizo zinahusiana na mashirika ya wahalifu yenye uhusiano na makundi ya kigaidi.

Lakini kwa mujibu wa Patrice Ribeiro wa chama cha Polisi (Syndicat de Police Synergie Officiers), ripoti hii ni chanya zaidi kuliko inavyoonekana. "Kumekuwa tangu mwanzo wa hali ya tahadhari zaidi ya upekuzi 3000 na taratibu 500 ambazo zilishughulikiwa haraka. Kuhusu vitendo vya ugaidi, ambavyo ni vigumu kuelezea, kumekuwa na taratibu kadhaa, idadi kubwa imekuwa taratibu za uhalifu mkubwa, uhalifu wa uliopangwa, ambayo yanahusiana na masuala ya madawa ya kulevya au biashara ya silaha. Lakini yote yanahusiana na ugaidi kwa sababu Waislam mara nyingi wanatokea katika maeneo ya uhalifu mkubwa, ambayo hutumiwa kuendelea Uislam, " Patrice Ribeiro amesema.

Dhana zisiokua na msingi kwa kutekeleza upekuzi

Hata hivyo wengi wana mashaka juu ya ufanisi wa Utaratibu huui. Dominique Curis kutoka shirika la kimataifa la Haki za binadamu Amnesty International anasema hivi: "Suala la ufanisi linajitokeza, wakati tunaona kwamba watu waliwekwa hatarini na kutuhumiwa katika masuala ambayo hayahusiani na mapambano dhidi ya ugaidi. Inaonekana kwamba utaratibu wa vikosi vya usalama wakati mwingine ulitumiwa kwa malengo mengine kuliko mapambano dhidi ya ugaidi. "

Dominique Curis ana wasiwasi hasa juu ya dhana zisiokua na msingi zilizobainishwa kwa kutekeleza upekuzi au kuopewa kifungo cha nyumbani.

Maswali mengi yameibuka juu ya kuongezwa muda kwa hali hii ya tahadhari nchini Ufaransa, licha ya serikali kujitetea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.