Pata taarifa kuu
URUSI-UTURUKI-UHASAMA-USALAMA

Vikwazo vya Urusi vinahusu mazao ya kilimo Uturuki

Vikwazo vilivyowekwa na Urusi dhidi ya Uturuki kufuatia kisa cha kuiangusha moja ya ndege zake za kivita iliyokua ikiendesha shughuli zake nchini Syria vitahusu tu mazao ya kilimo na huenda vikaanza kutekelezwa kwa majuma kadhaa, maafisa wa Urusi wametangaza Jumatatu wiki hii.

Vikwazo vya Urusi dhidi ya Uturuki vitalenga tu mazao ya kilimo.
Vikwazo vya Urusi dhidi ya Uturuki vitalenga tu mazao ya kilimo. REUTERS/Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

Naibu Waziri mkuu Arkady Dvorkovich amesema wakati wa mkutano wa serikali kwamba Moscow inaweza kuchelewesha utekelezaji wa vikwazo hivyo vinavyolenga matunda na mboga ili kutoimarisha mfumuko wa bei unaoshuhudiwa Urusi.

Mamlaka ya Urusi tayari imepiga marufuku uagizaji wa bidhaa za kilimo kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na vikwazo vilivyopitishwa na Umoja huo kutokana na vita vinavyoendelea mashariki mwa Ukraine.

Naibu Waziri Mkuu wa kwanza Igor Shuvalov, amesema kwa upande wake kwamba kwa sasa Moscow haitopiga marufuku uagizaji wa bidhaa za viwandani kutoka Uturuki.

Waziri mkuu Dmitry Medvedev ameonya, hata hivyo, wakati wa mkutano huo kuwa vikwazo vilivyotangazwa Jumamosi vinaweza kupunguzwa baadaye "kama itahitajika".

Athari za vikwazo zimeanza kuonekana kwa wafanyabiashara wa Uturuki wanaosafirisha bidhaa zao nje ya nchi hiyo. Malori 1,250 yanayosheheni bidhaa za Uturuki zimezuiliwa katika nchini Georgia na Ukraine, nchi mbili ambazo wanapaswa kupita kabla ya kuingia nchini Urusi, afisa wa Uchukuzi wa Urusi ameliambia shirika la habari la Uingereza la Reuters Jumatatu wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.