Pata taarifa kuu
URUSI-UTURUKI-UHASAMA-USALAMA

Vita vya maneno kati ya Uturuki na Urusi vyaendelea

Alhamisi hii Novemba 26, Uturuki imetetea wazi ahadi yake "isiyopingwa" dhidi ya wanajihadi katika kukabiliana na shutuma za Urusi na kupinga kuiomba msamaha baada ya moja ya ndege zake za kivita kuangushwa kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisema kuwa hawezi kuomba msamaha kwa tuhuma za Urusi za kuwa na mahusiano na Kundi la Islamic State.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisema kuwa hawezi kuomba msamaha kwa tuhuma za Urusi za kuwa na mahusiano na Kundi la Islamic State. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa hotuba yake jijini Ankara, Rais Recep Tayyip Erdogan amekanusha madai kuwa nchi yake imekua ikiwapa nafasi ya kupitia au kufaidika na mauzo ya mafuta ya Islamic State (IS).

"Wale wanaotushtumu kwa kununua mafuta ya Kundi la Islamic State wana wajibu wa kuthibitisha madai yao. Kama siyo, ni wasingiziaji", Rais Erdogan amesema mbele ya maafisa wa serikali.

"IS inauza mafuta inayochimba kwa Assad", Erdogan amesema, akimaanisha rais wa Syria Bashar al-Assad, "zungumza suala hilo na Assad ambaye unaunga mkono", Rais wa Uturuki ameongeza.

Ankara na Moscow zinatofautiana juu ya suala la Syria. Uturuki inataka Assad aondoke madarakani kama sharti lilsilopingwa kwa suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa Syria, wakati ambapo Urusi na Iran, wameendelea kumuunga mkono Bashar Al Assad.

Uhusiano wa nchi hizi mbili umedorora mno tangu kuangushwa kwa ndege ya kijeshi ya Urusi Jumanne wiki hii.

Uturuki inadai kuwa iliidungua ndege ya Urusi Su-24 kwa sababu ilikiuka sheria na kuingia katika anga yake, baada ya kuonywa mara kumi. Urusi imesema badala yake kwamba ndege yake haikuingia katika anga ya Uturuki na wala haikuonywa kabla ya kudunguliwa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameitaka Urusi kuomba radhi, baada ya kuwatuhumu viongozi wa nchi hiyo kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.