Pata taarifa kuu
URUSI-UTURUKI-UHASAMA-USALAMA

Urusi yaishushia lawama Uturuki baada ya ndege yake kudunguliwa

Jumatano wiki hii, Urusi imeishtumu Uturuki kuanzisha "uchochezi uliyopangwa" siku moja baada ya kulipuliwa kwa ndege yake ya kivita, karibu na mpaka wa Syria, huku viongozi wa Urusi wakiweka kando, kama Ankara, kuongezeka kwa uhasama wa kijeshi katika Ukanda huo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akiionyooshea kidole cha lawama Uturuki, siku moja baada ya ndege yake ya kijeshi kuangushwa na jeshi la Uturuki.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiionyooshea kidole cha lawama Uturuki, siku moja baada ya ndege yake ya kijeshi kuangushwa na jeshi la Uturuki. Russian President Vladimir Putin takes part in a live broadcast
Matangazo ya kibiashara

"Tuna mashaka makubwa kuwa ni kitendo kiliotekelezwa kwa maksudi, yote hayo yanaonyesha kuwa ni uchochezi uliyopangwa", Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov Waziri amesema katika mkutano wa waandishi wa habari.

Hata hivyo, Urusi "haitaingia vitani dhidi ya Uturuki, mahusiano yake na raia wa Uturuki hayakubadilika", Lavrov amesema.

Kwa upande wake, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amehakikisha kuwa hakuna nia yoyote ya kuanzisha uhasama baada ya tukio hilo la kuangushwa kwa ndege ya kijeshi ya Urusi, na Waziri mkuu Ahmet Davutoglu amesema kuwa Ankara ilikuwa "rafiki na jirani" wa Urusi.

Jumanne wiki hii, ndege ya kijeshi ya Urusi Su-24 ilidunguliwa na ndege mbele za jeshi la Uturuki F-16. Ankara imesema kuwa ndege hiyo ilikua katika anga ya Urus, wakati ambapo Moscow imebaini kwamba ndege yake ya kivita ilidunguliwa ikiwa katika anga ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.