Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Zaidi ya watu mia moja wauawa katika mashambulizi ya kigaidi Paris

Angalau watu 120 wameuawa na zaidi ya 200 wamejeruhiwa Ijumaa jioni wiki hii katika mfululizo wa kipekee wa mashambulizi ya kigaidi mjini Paris na karibu na Uwanja taifa wa michezo (Stade de France), pamoja na mara ya kwanza nchini Ufaransa vitendo vya kujitoa mhanga, hasa katika ukumbi wa tamasha wa Bataclan.

Mwathirika wa mashambulizi ya ukumbi wa tamasha wa Bataclan mjini Paris wakiondolewa na maafisa wa dara ya huduma za dharura, Novemba 14, 2015.
Mwathirika wa mashambulizi ya ukumbi wa tamasha wa Bataclan mjini Paris wakiondolewa na maafisa wa dara ya huduma za dharura, Novemba 14, 2015. KENZO TRIBOUILLARD/AFP
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji wanane wamepoteza maisha, ikiwa ni pamoja na saba kati yao walijilipua.

Bataclan, ambapo idadi kubwa ya watu walipoteza maisha, "kulikuwa na damu kila mahali, miili ya watu waliouawa kila mahali", "kulisikika kelele, kila mtu alijaribu kukimbia, huku watu wakikanyagana. Ilikuwa kama Kiyama", mashahidi wa kwanza wameeleza.

Ukubwa wa janga hili umeuweka mji mkuu katika katika hali ya hatari, zikiwa zimesakliwa zaidi ya wiki mbili za ufunguzi wa mkutano kuhusu tabia nchi (COP21) katika mji wa Bourget, kaskazini mwa Paris, ambapo wanasubiriwa mamia ya marais na viongozi wa Serikali.

Kwa ujumla, watu wasiopungua 120 wameuawa na zaidi ya 200 wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na 80 ambao wamejeruhiwa vibaya, chanzo kilio karibu na uchunguzi kimesema.

Ofisi ya mwendesha mashitaka imeanzisha uchunguzi wa mauaji katika uhusiano na kundi la kigaidi ili kutoa mwanga juu ya mashambulizi haya yaliosababisha vifo vya watu wengi Ulaya ya Magharibi katika miaka arobaini ya hivi karibuni baada ya mashambulizi ya Madrid yaliotokea mwezi Machi 2004. Uchunguzi utaruhusu kujua kama bado "washirika au baadhi ya waliohusika na mashambulizi hayo bado wapo nchini Ufaransa", mwendesha mashitaka wa mji wa Paris, François Molins amesema.

"Wakati huu ni vita", ni kichwa cha habari kwenye gazeti la kila siku la Le Parisien kwa habari iliyochapishwa Jumamosi hii asubuhi, miezi kumi baada wimbi la mashambulizi katika mji wa Paris.

Washambuliaji wanne wamefariki katika ukumbi wa tamasha wa Bataclan, ikiwa ni pamoja na watatu waliojilipua, na wa mwisho ameuawa wakati wa operesheni ya vikosi vya usalama. Katika Uwanja wa taifa wa michezo (Stade de France), watu wa kujitoa mhanga watatu walifariki, na mwingine kwenye barabara kuu ya Voltaire.

Katika mji wa Bataclan, operesheni imeendeshwa "haraka sana kwa sababu watu wengi wangeliuawa", chanzo kilio karibu na uchunguzi kimebaini. Wahusika wa mashambulizi hayo wamebaini kwamba ni ulipizaji kisasi kwa uingiliaji kati kijeshi wa Ufaransa nchini Syria, shahidi mmoja ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.