Pata taarifa kuu
SENEGAL-UFARANSA-MAUAJI-CHARLIE HEBDO-JAMII

Usambazaji wa toleo la Charlie Hebdo wapigwa marufuku

Waziri wa mambo ya ndani wa Senegal amepiga marufuku usambazaji nchini Senegal wa toleo la wiki hii la jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo lililoshambuliwa juma lililopita mjini Paris nchini Ufaransa.

Rais wa Senegal, Macky Sall akiwa na rais wa Ufaransa, François Hollande Januari 11 kabla ya maandamano ya kitaifa, mjini Paris.
Rais wa Senegal, Macky Sall akiwa na rais wa Ufaransa, François Hollande Januari 11 kabla ya maandamano ya kitaifa, mjini Paris. AFP PHOTO / DOMINIQUE FAGET
Matangazo ya kibiashara

Kibonzo cha Mtume Muhammad kimewekwa katika ukurasa wa mbele wa toleo hilo, akiwa na bango lenye maandishi “Je suis Charlie, tout es pardonné”, ikimaanisha “mimi ni charlie nimesamehe yote.”

Shirika la habari la Senegal limebaini kwamba magazeti ya jarida hilo la Chalie Hebdo yalipigwa marufuku kuzambazwa nchini Senegal tangu miaka miwili iliyopita, lakini yanapatikana tu katika baadhi ya maktaba.

 

Hata hivyo rais wa Senegal, Macky Sall, aliungana Jumapili Januari 11 mwaka 2015, na rais wa Ufaransa pamoja na raia wa taifa hilo katika maandamano ya kupinga mauaji ya watu 12 wakati wa shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.

Wakati huo rais Macky Sall alilaumiwa na wanasiasa pamoja na viongozi wa kidini kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Wengi waliona kwamba kitendo hicho cha rais cha kuungana katika maandamano hayo ni kufuru, wengine wakiona kuwa ni kuiunga mkono Ufaransa kwa kuukashifu Uislam.

Toleo hilo la wiki hii la jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo limechukuliwa nchini Senegal kama uchokozi dhidi ya Uislam.

Kwa mujibu wa chanzo cha wizara ya mambo ya ndani, kama rais Macky Sall alijielekeza Paris, ni “ kuonyesha heshima kwa maisha ya binadamu”. Na kama amechukua uamzi wa kupiga marufuku usambazaji wa toleo hilo la Charile Hebdo ni "kuonyesha heshima kwa imani ya Uislam", kimeendelea kusema chanzo hicho.

Hata gazeti lingine la Ufaransa Libération limepigwa marufuku nchini Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.