Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-Maandamano

Maandamano ya kihistoria Ufaransa

Takribani viongozi 56, ikiwa ni pamoja na marais 44 wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na Ulaya, wamekutana Jumapili Januari 11 mjini Paris kwa kuonesha umoja wao.

Maandamano kwa heshima ya waathirika wa mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Paris.
Maandamano kwa heshima ya waathirika wa mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Paris. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wakishirikiana na raia wameandamana baada ya mashambulizi yaliyogharimu maisha ya watu zaidi ya 17 katika wiki hii mjini Paris.

Wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na rais wa sasa na mtangulizi wake, walijiunga na mamia ya maelfu ya raia, na kuandamana katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Kwa mujibu wa waandaaji wa maandamano hayo, watu kati ya milioni 1.3 na milioni 1.5 wameandamana mchana wa leo Jumapili.

Hii ni ishara ya kupiga vita ugaidi, baada ya watu wawili ndugu kushambulia Jumatano Januari 7 jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo na kuuwa watu 12 wakiwemo waandishi na askari polisi wawili. Alhamisi Januari 8 mtu mwengine mwenye silaha alivamia duka moja linalomilikiwa na Myahudi na kuwateka nyara watu waliokuwemo katika duka hilo.

Marais wa nchi za kigeni wakimzunguka rais wa Ufaransa, François Hollande wakati wa maandamano yaliyofanyika Januari 11 mwaka 2015.
Marais wa nchi za kigeni wakimzunguka rais wa Ufaransa, François Hollande wakati wa maandamano yaliyofanyika Januari 11 mwaka 2015. RFI/Pierre René-Worms

Wauaji hao waliuawa baada ya vikosi vya usalama kuendesha operesheni kabambe katika maeneo walipokuwa wamejificha.

Awali Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve amesema kuwa " mamia kwa maelfu ya watu wanatarajiwa" kushiriki katika maandamano ya kitaifa ambapo yalipangwa kuanza saa tisa saa za Ufaransa (sawa na saa nane saa za kimataifa).

Barabara mbili zimetengwa kwa maandamano hayo na ulinzi umeimarishwa. Maandamano hayo yataanzia eneo la Jamhuri hadi eneo la Taifa.

Wakati wa maandamano hayo makubwa, vikosi vya usalama vimechukua tahadhari ya mambo mawili ambayo ni muhimu kwa usalama wa waandamanaji : kutokubali gari kuingia msafara wa magari ya viongozi au vurugu zitakazochochewa na watu, kimethibitisha chanzo cha polisi.

Vitengo ishirini na nne vya vikosi vya usalama sawa na askari polisi 2,200 wamekua wamewekwa tayari kutoa ulinzi katika maandamano hayo. Aidha, askari polisi 2,000 na wanajeshi 1,350 wameshiriki katika mpango wa ulinzi dhidi ya ugaidi , ikiwa ni pamoja na kulinda maeneo muhimu: makao makuu ya vyombo vya habari, maeneo ya kuabudu, shule za dini, majengo ya serikali na balozi mbalimbali katika mji wa Paris na vitongoji vyake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.