Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-Maandamano

Usalama waimarishwa kwa ajili ya maandamano ya kihistoria Paris

Hatua za kipekee za usalama zimepitishwa kwa ajili ya maandamano ya kipekee Jumapili Januari 11 katika mji wa Paris.

Jeshi lapiga doria mbele ya mnara wa Eiffel mjini Paris, Januari 10 mwaka 2015.
Jeshi lapiga doria mbele ya mnara wa Eiffel mjini Paris, Januari 10 mwaka 2015. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Mamia kwa maelfu ya watu na marais pamoja na viongozi wa serikali zaidi ya hamsini watashiriki katika maandamano hayo, kwa heshima ya waathirika wa mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Paris.

Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve amechukua uamzi mwenyewe Jumamosi Januari 10 alaasiri wa kuandaa kikosi cha " kipekee" kwa ajili ya maandamano hayo makubwa.

Waziri Cazeneuve amesema kuwa " mamia kwa maelfu ya watu wanatarajiwa" kushiriki katika maandamano ya kitaifa ambapo yamepangwa kuanza saa tisa saa za Ufaransa (sawa na saa nane saa za kimataifa).

Barabara mbili zimetengwa kwa maandamano hayo na ulinzi umeimarishwa. Maandamano hayo yataanzia eneo la Jamhuri hadi eneo la Taifa.

Wakati wa maandamano hayo makubwa, vikosi vya usalama vitachukua tahadhari ya mambo mawili ambayo ni muhimu kwa usalama wa waandamanaji : kutokubali gari kuingia msafara wa magari ya viongozi au vurugu zitakazochochewa na watu, kimethibitisha chanzo cha polisi.

Vitengo ishirini na nne vya vikosi vya usalama sawa na askari polisi 2,200 wamewekwa tayari kutoa ulinzi katika maandamano hayo. Aidha, askari polisi 2,000 na wanajeshi 1,350 watashiriki katika mpango wa ulinzi dhidi ya ugaidi , ikiwa ni pamoja na kulinda maeneo muhimu: makao makuu ya vyombo vya habari, maeneo ya kuabudu, shule za dini, majengo ya serikali na balozi mbalimbali katika mji wa Paris na vitongoji vyake, ameeleza Waziri Cazeneuve.

Wanahabari waandamana Burundi

Nchini Burundi vyma vya waandishi wa habari vimepanga kukusanyika mbele ya ubalozi wa Ufaransa mjini Bujumbura ili kuungana na raia wa Ufaransa waishio nchini Burundi kwa heshima ya waathirika wa mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Paris, hususan shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu 12 wakiwemo wachoraji wa vibonzo na askari polisi.

Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha waandishi wa habari UBJ nchini Burundi, Alexandre Niyungeko, shambulio dhidi ya jarida la Charlie Hebdo lililogharimu maisha ya watu 12 ni pigo kubwa kwa jamii ya wanahabari wa Burundi.

Maandamano katika mji wa Marseille, Januari 10 mwaka 2015.
Maandamano katika mji wa Marseille, Januari 10 mwaka 2015. REUTERS/Philippe Laurenson

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.