Pata taarifa kuu

Ufaransa yaandamana kwa amani kuwakumbuka waathirika wa mashambulizi

Takribani watu laki saba wamejitokeza katika maandamano nchini Ufaransa kufuatia siku tatu za mashambulizi yaliyosababisha mauaji katika maeneo ya jiji la Paris.

Maandamano ya amani yafanyika Ufaransa kuwakumbuka waathirika wa mashambulizi ya hivi karibuni mjini Paris
Maandamano ya amani yafanyika Ufaransa kuwakumbuka waathirika wa mashambulizi ya hivi karibuni mjini Paris AFP PHOTO / PASCAL PAVANI
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalishuhudiwa katika miji sita ya nchi hiyo kutoa heshima kwa watu walioathirika na mashambulizi ya juma lililopita.

Watu kumi na saba waliuawa katika mashambulizi yaliyotekelezwa katika makao makuu ya jarida la vibonzo Charlie hebdo ,maafisa polisi,na wengine katika duka la jumla.

Polisi wanaendelea kuwasaka washirika wa washambuliaji watatu ambao waliuawa na polisi.

Wizara ya mambo ya ndani imearifu kuwa nchi hiyo itakuwa katika tahadhari ya hali ya juu kiulinzi katika majuma kadhaa yajayo.

Wakati wa maandamano kulikuwa na saa ya ukimya,wengine wakibeba mabango yenye jumbe mbalimbali kama Umoja au mimi ni charlie ikimaanisha jarida la vibonzo ambalo waandishi wake walishambuliwa na ndugu wawili waliokuwa na silaha jumatano.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.