Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-USALAMA

Uturuki: mchakato wa amani na PKK hatarini

Nchini Uturuki, siku mbili baada ya mashambulizi katika mji wa Suruç kuhusishwa kundi la Islamic State, mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 32 na kujeruhi mamia wengine, kundi la waasi wa Kikurdi limekiri Jumatano wiki hii kuwaua askari polisi wawili wa Uturuki. Hatua ambayo inaweza kuvunja mchakato wa amani.

Waandamanaji wanashikilia bendera, ikiwa ni pamoja na ile ya PKK, na picha za wahanga wa mashambulizi ya Suruç wakati wa mazishi katika mji wa Istanbul tarehe 22 Julai.
Waandamanaji wanashikilia bendera, ikiwa ni pamoja na ile ya PKK, na picha za wahanga wa mashambulizi ya Suruç wakati wa mazishi katika mji wa Istanbul tarehe 22 Julai. Reuters/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Ni katika tovuti ya HPG, tawi la kijeshi la PKK,ambapo kundi hili limedai kuwaua askari polisi wawili wa Uturuki. Kundi hilo limesema "hatua za adhabu zilizochukuliwa dhidi ya maofisa wawili wa polisi ambao waliku wakishirikiana na kundi la Daech [kundi la Islamic State]." Leo, mchakato wa amani unaoendelea kwa muda wa miaka mitatu unaonekana kuwa hatarini. Hasa kwa vile vita kati ya Wakurdi na wanajihadi nchini Syria na Iraq bila hata hivyo serikali ya Ugiriki kuingilia kati imesababisha chuki kali miongoni mwa raia wa Kikurdi nchini Uturuki. Na shambulio lililotokea hivi karibuni katika mji wa Suruç, limezua hisia kubwa.

Shambulio hili lilisababisha vifo vya watu 32 na mamia watu kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni vijana wafuasi wa chama cha kisoshalisti wenye umri uliyo kati ya ishirini na kuendelea. Walikuwa wamekusanyika katika mji wa Suruç kwa mwito wa Shirikisho la vijana wa Kisoshalisti nchini Uturuki wakiwa na lengo la kushiriki katika ujenzi wa mji wa Syria wa Kobani, upande wa pili wa mpaka.

Picha za wahanga wzilizunguka duniani kote. Mmoja wao, alikua daktari wa watoto wachanga ambaye alikua hana muda mrefu anamaliza chuo.

Serikali ya Uturuki inatuhumiwa kusaidia IS

Suruç ni mji wa Kikurdi wenye wakazi 50,000 ambao unapatikana kaskazini mwa Kobani, ishara kwa Wakurdi tangu walipoutwaa mji huo kutoka mikononi mwa kundi Islamic State. Shambulio la Suruçlililenga hasa Wakurdi.

Jamii ya watu hao pia inapatikana nchini Syria, Iran na Iraq, Wakurdi wanaunda ni asilimia 20 ya wakazi nchini Uturuki. Tangu Wakurdi wa Iraq walipopata mafanikio ya kujitegemea, serikali ya Uturuki ina hofu ya kuvunjika kwa taifa la Uturuki. Wakurdi wanamtuhumu rais Recep Tayyip Erdogan na chama tawala kuunga mkono wanajihadi dhidi ya wapiganaji Kikurdi nchini Syria. Tuhuma ambazo zimefutiliwa mbali na Ankara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.