Pata taarifa kuu
UTURUKI-UCHAGUZI-SIASA

Uturuki: chama cha HDP chaingia bungeni

Nchini Uturuki, kwa mujibu wa matokeo kuhusu kura zote zilizohesabiwa, chama cha kihafidhina cha kiislamu cha AKP cha rais Erdogan kimeshinda uchaguzi wa wabunge lakini kimepoteza wingi wa viti bungeni ambapo, chama kinachounga mkono Wakurdi cha HDP kimepata asilimia13 ya kura.

Wafuasi wa chama cha HDP wanasheherekea kura ambazo chama chao kimepata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge Juni 7 mwaka 2015.
Wafuasi wa chama cha HDP wanasheherekea kura ambazo chama chao kimepata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge Juni 7 mwaka 2015. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Kwa matokeo haya chama cha HDP kimeingia bungeni. Viongozi wa chama hiki waliendesha mkutano na waandishi wa habari, baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi. Viongozi hawa waliwashukura watu waliojitolea na wale waliowasaidia katika kampeni zao za uchaguzi, huku wakilani mashambulizi kadhaa yaliyotokea majuma kadhaa yaliyopita.

Viongozi wa chama cha HDP waliahidi kufanya kiliyo chini ya uwezo wao kwa kuanzisha upya na kuendelea na mchakato wa amani kati ya Ankara na waasi wa Kikurdi, baada ya zaidi ya miaka 30 ya kuzuka kwa kundi la waasi na kuanzishwa kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Uturuki.

Chama cha HDP pia kimeahidi kutojiunga na chama cha kihafidhina cha kiislamu cha AKP chama cha rais Erdogan.

Chama cha HDP kitawakilishwa na wabunge 79 katika Bunge la Uturuki. Viongozi wa chama hiki wamekumbusha jinsi gani vita vya kisiasa vilipelekea chama caha HDP kupata asilimia 13 ya kura katika uchaguzi wa wabunge. Viongozi hao wamesema ushindi huo walioupata ni mkubwa mno kwa kubadilisha hali ya mambo nchini Uturuki.

Mbele ya mgahawa ambako viongozi wa chama cha HDP walifanya mkutano na waandishi wa habari, mamia ya wafuasi walikusanyika eneo hilo wakiimba udugu ulio kati ya Wakurdi na Waturuki, huku wakiwa na matumaini kuwa udugu huo ndio ulipelekea ushindi huo wa kihistoria unapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.