Pata taarifa kuu
UTURUKI-UCHAGUZI-SIASA

Uturuki : Serikali ya Davutoglu yajiuzulu

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekubali Jumanne wiki hii kujiuzulu kwa serikali ya Ahmet Davutoglu, huku mazungumzo kuhusu kuundwa kwa serikali mpya ya muungano yakiendelea vizuru, siku mbili baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge.

Rais wa UturukiRecep Tayyip Erdogan, Mei 29 mwaka 2015.
Rais wa UturukiRecep Tayyip Erdogan, Mei 29 mwaka 2015. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Ahmet Davutoglu na serikali yake watabaki mpaka pale serikali mpya itakapo tangazwa.

Kwa mujibu wa matokeo kuhusu kura zote zilizotangazwa, chama cha kihafidhina cha kiislamu cha AKP cha rais Erdogan kimeshinda uchaguzi wa wabunge lakini kimepoteza wingi wa viti bungeni ambapo, chama kinachounga mkono Wakurdi cha HDP kimepata asilimia13 ya kura.

Kwa matokeo haya chama cha HDP kimeingia bungeni. Hivi karibuni viongozi wa chama hiki waliendesha mkutano na waandishi wa habari, baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi. Viongozi hawa waliwashukura watu waliojitolea na wale waliowasaidia katika kampeni zao za uchaguzi, huku wakilani mashambulizi kadhaa yaliyotokea majuma kadhaa yaliyopita.

Chama cha HDP pia kimeahidi kutojiunga na chama cha kihafidhina cha kiislamu cha AKP chama cha rais Erdogan.

Chama cha HDP kitawakilishwa na wabunge 79 katika Bunge la Uturuki. Viongozi wa chama hiki wamekumbusha jinsi gani vita vya kisiasa vilipelekea chama caha HDP kupata asilimia 13 ya kura katika uchaguzi wa wabunge. Viongozi hao wamesema ushindi huo walioupata ni mkubwa mno kwa kubadilisha hali ya mambo nchini Uturuki.

Mbele ya mgahawa ambako viongozi wa chama cha HDP walifanya mkutano na waandishi wa habari, mamia ya wafuasi walikusanyika eneo hilo wakiimba udugu ulio kati ya Wakurdi na Waturuki, huku wakiwa na matumaini kuwa udugu huo ndio ulipelekea ushindi huo wa kihistoria unapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.