Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Mapigano

Ndege ya kijeshi ya Ukraine yadunguliwa, Moscow yanyooshewa kidole

Hali ya taharuki inaendelea kutanda mashariki mwa Ukraine, ambapo jeshi la nchi hio linaendelea na operesheni yake dhidi ya waasi kwa lengo la kurejesha kwenye himaya yake miji inayoshikiliwa na waasi, hususan mji wa Lougansk, ambapo mapigano yanaendelea kurindima.

Mabaki ya ndege ya Ukraine aina ya An-26 karibu na kijiji cha Davido-Nikolsk katika eneo la Lougansk.
Mabaki ya ndege ya Ukraine aina ya An-26 karibu na kijiji cha Davido-Nikolsk katika eneo la Lougansk. PHOTO/ STEPHANE ORJOLLET
Matangazo ya kibiashara

Hayo yakijiri ndege ya kijeshi ya Ukraine imedunguliwa, wakati operesheni ya kurejesha kwenye himaya ya jeshi miji inayoshikiliwa na waasi ikiendelea. Zoezi la kutafuta mabaki ya ndege hio imeanza, huku Kiev ikiituhumu Moscow kuhusika na na kitendo hicho.

Waasi wanamiliki zana nzito nzito za kijeshi hususan makombora ya aina mbalimbali, lakini zana hizo hazina uwezo wa kudungua ndege inayopaa kwenye umbali wa mita 6500. Makombora yalirushwa yakutokea kwenye aridhi ya Urusi. Hayo ni madai yanayotolewa na ikulu ya Ukraine, ikibaini kwamba ni uchunguzi uliyoendeshwa na wizara ya ulinzi. Kwa mujibu wa msemaji wa jesji la Ukraine, ndege hiyo ilishambuliwa na kombora aina ya Pantsir X-24-air linaloaminiwa kuwa lilirushwa na ndege ya Urusi iliyokuwa ikitokea kwenye uwanja wa ndege wa Millerovo.

Ndege hiyo ya jeshi la Ukraine ilidondoka karibu na kijiji cha eneo la Lougask, karibu na mpaka wa Urusi. Baadhi ya wanajeshi waliokuwemo ndani ya ndege hio wamefaulu kuruka hadi aridhini, na wamejaribu kuwasiliana na makao makuu ya jeshi la Ukraine. Hadi sasa haijulikani idadi ya wanajeshi waliokua ndani ya ndege hio aqina ya Antonov 26.

Shambulio la ndege hii ni pigo kubwa kwa jeshi la Ukraine ambalo limekua likijaribu kurejesha kwenye himaya yake mji wa Lougansk, kwenye umbali wa kilomita zaidi ya hamsini mbali kidogo na magaribi mwa taifa hilo.

Hivi karibuni jeshi lilmekua limefaulu kureshesha kwenye himaya yake baadhi ya maeneo na kutangaza kufungua uwanja wa ndege uliyokua ukishikiliwa kwa majuma kadhaa na waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.