Pata taarifa kuu
UKRAINE-Usalama-Siasa

Wanajesji 23 wa Ukraine wauawa katika mapigano

Jeshi la Ukraine limewapoteza wanajeshi wake 23 ambao wameuawa katika mapigano na waasi mashariki mwa Ukraine kwa muda wa saa 24, amesema msemaji wa jeshi.

Kifaru cha jeshi la Ukraine katika mji wa Sloviansk, muda mchache baada ya kutekwa na waasi.
Kifaru cha jeshi la Ukraine katika mji wa Sloviansk, muda mchache baada ya kutekwa na waasi. REUTERS/Maria Tsvetkova
Matangazo ya kibiashara

Waasi wakiwa wakiwa karibu ya eneo ilikodunguliwa ndege ya jeshi la Ukrianekatika mji wa Lougansk.
Waasi wakiwa wakiwa karibu ya eneo ilikodunguliwa ndege ya jeshi la Ukrianekatika mji wa Lougansk. REUTERS/Shamil Zhumatov

Vladyslav Seleznov, msemaji wa “operesheni inayopambana dhidi ya ugaidi”,ambayo inaendeshwa na jeshi la Ukraine amekanusha habari isiyo sahihi kuhusu idadi ya wanajeshi 30, ambao huenda waliuawa kwa mashambulizi mfululizo ya makombora, ambayo imekua ikitangazwa na kuonyeshwa kwenye radio na televisheni, ambazo hakuzitaja.

Vladyslav Seleznov, amesema kwa jumla wanajeshi 93 wameuawa katika mapigano hayo kwa muda mfupi katika maeneo yote kunakoripotiwa mapigano.

Hayo yakijiri Umoja wa Ulaya umeongeza kwenye orodha yake majina 11 ya watu wanaolengwa na vikwazo viliyowekewa watu wanaohusika katika mzozo wa Ukraine, hususan wanaoendelea kukuza mzozo huo mashariki mwa Ukraine.

Majina hayo yatatangazwa jumamosi wiki hii kwenye gazeti la Umoja wa Ulaya. Idadi ya wanaolengwa na vikwazo hivyo imefikia sasa 61. Watu hao wanakabiliwa na vikwazo vya kusafiri na kuzuiliwa kwa mali zao.

Mapigano yanaendelea mashjariki mwa Ukraine kati ya jeshi na waasi.
Mapigano yanaendelea mashjariki mwa Ukraine kati ya jeshi na waasi. REUTERS/Yannis Behrakis

Wakati huo huo mapigano yanapamba moto katika mji wa Donetsk, ambapo jeshi limeongeza mashambulizi kwa lengo la kuteka mji huo, huku waasi wakizidisha nguvu kwa lengo la kurejesha nyuma jeshi la serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.