Pata taarifa kuu
PARALYMPIC 2016-RIO

Michezo ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu yafana, waandaaji wapongezwa

Michezo ya Olimpiki ya Rio kwa watu wenye ulemavu imefikia tamati mwishoni kwenye uwanja wa Maracana, huku watu wengi wakipongeza namna ambavyo michezo ya mwaka huu imefanikiwa licha ya hali ya kisiasa nchini Brazil.

Baadhi ya wanamichezo wenye ulemavu wakiwa wamebeba bendera zao wakati wa sherehe za kufungwa michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016, Brazil. 18 September, 2016.
Baadhi ya wanamichezo wenye ulemavu wakiwa wamebeba bendera zao wakati wa sherehe za kufungwa michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016, Brazil. 18 September, 2016. REUTERS/Sergio Moraes
Matangazo ya kibiashara

Waimbaji, wacheza mziki na milipuko ya fataki ilipamba sherehe za ufungwaji wa michezo hiyo ya aina yake, ambapo kabla maelfu ya washiriki na watazamaji walishiriki kutoa heshima za mwisho kwa mwanamichezo wa Iran, Bahman Golbarnezhad, aliyefariki siku ya Jumamosi.

Rais wa kamati ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu, Sir Philip Craven, akizungumza wakati wa ufungwaji wa michezo ya mwaka huu, amesema kuwa ilikuwa ni michezo ya kufana licha ya simanzi iliyotokana na kifo cha mwanamichezo mmoja.

Akizungumzia mafanikio ya michezo ya mwaka huu ya Rio, Craven amesema michezo ya mwaka huu ilikuwa ya “aina yake kwa Brazil na imeshangaza wengi,” alisema Rais huyo.

Philip Craven, rais wa kamati ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu, akihutubia wakati wa ufungwaji wa michezo ya mwaka huu jijini Rio, Brazil, 18 September, 2016.
Philip Craven, rais wa kamati ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu, akihutubia wakati wa ufungwaji wa michezo ya mwaka huu jijini Rio, Brazil, 18 September, 2016. REUTERS/Ricardo Moraes

Uingereza ilimaliza michezo hiyo ikiwa na medali 147, huku medali 61 zikiwa ni za dhahabu, ambapo ilikuwa ya pili nyuma ya Uchina ambayo ilipata medali 107 za dhahabu na kumaliza ikiwa na jumla ya medali 239.

Craven aliwashukuru waandaaji, wanamichezo na watazamaji baada ya kukabidhi bendera ya Paralympic kwa gavana wa jiji la Tokyo, ambayo itaandaa michezo ijayo ya Olimpiki ya mwaka 2020.

Akiwa amesimama kando na Craven, Carlos Nuzman, Rais wa kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya rio, alishangiliwa pale aliposema kuwa “Misheni imekamilika” akimaanisha kuwa jukumu ililokuwa imepewa nchi yake, limemalizika kwa mafanikio.

Alisema kuwa “Brazil tunayoipenda sana imeonesha dunia kuwa inaweza kufanya”, michezo hii “ilianza kama ndoto, ilikuwa ni miaka 20 toka maandalizi yake, wengi walidhania kuwa itashindikana, lakini sio kwa Rio na Brazil,” alisema rais huyo wa kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Brazil.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.