Pata taarifa kuu
KYRGHYZISTAN-MICHEZO

Izza Artykov afukuzwa katika mashindano ya Rio-2016

Mwanariadha wa nchi ya Kyrghyzistan, Izza Artykov, amefukuzwa katika michezo ya Olimpiki inayoendelea katika mji wa Brazil wa Rio de Janeiro, baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa alikua akitumia madawa ya kusismu misuli.

Wanamichezo waendelea kufukuzwa katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro 2016.
Wanamichezo waendelea kufukuzwa katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro 2016. REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na uamuzi huo, Izza Artykov amepoteza medali ya shaba alioshindia katika kundi la watu wanaopima uzito uliyo chini ya kilogramu 69.

Uamuzi wa kufukuzwa kwa Izza Artykov umechukuliwa na Mahakama ya michezo, iliyoombwa kwa mara ya kwanza na Kamati ya Olimpiki kuhukumu kesi ya matumizi ya madawa ya kusisimua mwili katika hatua ya mwanzo.

Kyrgyz ambaye alibeba vitu vyenye uzito wa jumla ya kilo 339, alichukua nafasi ya 3 Agosti 10.

Mchina Shi Zhiyong Shi ndiye aliiibuka mshindi, baada ya kumsinda Mturuki Daniyar Ismayilov (kilogramu 351).

Kwa miaka mingi, Izza Artykov alidhoofishwa na matumizi ya madawa ya kusisimu mwili.

Mbulgaria, amayejulikana kama bibi wa nidhamu amepigwa marufuku kushiriki mashindano hayo kwa kosa la matumizi ya madawa ya kusisimua mwili.

Wanamichezo wanane kutoka Urusi waliofuzu kwa mashindano ya Michezo ya Olimpiki katika mji wa Rio de Janeiro wamewekwa kando kufuatia ripoti ya McLaren ya Julai 18, inayoonyesha hali ya matumizi ya madawa ya kusisimua mwili yanayofadhiliwa na serikali.

Agosti 6, mwanamichezo kutoka Cyprus, Antonis Martasides, alifanyiwa vipimo na kugundulika kuwa alikua kitumia madawa ya kusisimua mwili, na hivyo kufukuzwa kufukuzwa katika ujumbe wa nchi yake katika mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.