Rio 2016-KENYA
Kenya yapata medali ya kwanza ya dhahabu ya wanariadha walemavu
Mwanariadha mlemavu wa Kenya amejinyakulia medali ya dhahabu ya Michezo ya Olimpiki ya walemavu inayoendelea katika mji wa Rio de Janeiro, Nchini Brazil.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Afrika imerudi kupata sifa kupitia Kenya, katika michezo ya kimataifa, inayowakutanisha wanariadha mbalimbali duniani.
Samwel Kimani, ambaye ni kipofu ameibuka mshindi katika mbio za mita 5000 katika hatua ya T11 ya michezo ya riadha (mbio za vipofu wakiongozwa na kijiti).
Samwell Kimani mshindia medali ya pili ya dhahabu tangu kushiriki michezo hii ya kimataifa baada Mashindano ya mjini London mwaka 2012.