Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RIADHA

Kenya yamwagiza kocha wake wa mbio fupi kurudi nyumbani

Kenya imemwagiza kocha wa timu ya taifa ya riadha anayehusika na mbio fupi John Anzrah, kurejea nyumbani mara moja baada ya kudaiwa kukeuka utaratibu wa kuwachunguza wanariadha kubaini ikiwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu mwili.

Kocha John Anzrah
Kocha John Anzrah citizentv
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Michezo ya Olimpiki IOC imethibitisha kurudishwa nyumbani kwa kocha huyo na kuishukuru Kamati ya Olimpiki ya Kenya kwa hatua hiyo ya haraka.

Kocha huyo anadaiwa alikwenda kuchua vipimo kama mwanariadha kinyume na utaratibu wa Shirika la Kimataifa linalopambana na matumizi ya dawa hizi WADA na Shirikisho la riadha duniani IAAF.

Kamati ya Olimpiki nchini Kenya na ile ya Kimataifa inachunguza madai dhidi ya kocha huyu, ikiwa itabainika kuwa kweli atachukuliwa hatua.

Sakata hili linakuja siku kadhaa baada ya Meneja wa timu hiyo ya Kenya Michael Rotich kurudishwa nyumbani kwa madai ya kuomba rushwa, ili kutoa taarifa mapema kuwasaidia wanariadha kuhusu vipimo vya kubaini ikiwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Amefikishwa Mahakamani na sasa amezuiwa ili polisi kumaliza uchunguzi dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.