Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RIADHA

Meneja wa timu ya riadha ya Kenya aagizwa kurudi nyumbani

Meneja wa timu ya taifa ya riadha ya Kenya inayoshiriki katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil, Michael Rotich, ameagizwa kurejea nyumbani baada ya kudaiwa kuitisha fedha ili kuwalinda wanariadha wa nchi hiyo wanaodaiwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku za kuwaongezea nguvu mwilini.

Meneja Michael Rotich (kulia) aliyechorewa mstari
Meneja Michael Rotich (kulia) aliyechorewa mstari The Times
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya uchunguzi wa Gazeti la Uingereza la The Sunday Times na Televisheni ya Ujerumani ARD, imeeleza kuwa Bwana Rotich aliitisha Pauni za Uingereza 10,000 sawa na Shilingi za Kenya Milioni 1.3 kutoka kwa wanariadha hao na kuwaahidi kuwa atakuwa anawapa taarifa mapema kuhusu uchunguzi dhidi yao.

Inaripotiwa kuwa vyombo hivyo viwili vya habari vilimrekodi kwa siri Meneja huyu akiwa katika kambi ya mazoezi ya Iten katika eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya.

Hizi ni habari mbaya sana kwa wanariadha wa Kenya ambao baadhi yao wamekuwa wakituhumiwa kutumia dawa hizo wakati huu wakiwa nchini Brazil kuithibitishia dunia kuwa wanaweza kushinda bila ya kutuma dawa hizo.

Siku ya Ijumaa, Rotich alitarajiwa kuwaongoza wanariadha wa Kenya kupita jukwaani katika ufunguzi wa Michezo hii ya Olimpiki lakini kwa sababu ya tuhma zinazomkabili hakuonekana.

Taasisi ya Kenya iliyoundwa hivi karibuni kupambana na matumizi ya dawa hizi zilizopigwa marufuku, imesema itachunguza madai haya na kumchukulia hatua ikiwa itabainika ni kweli alihusika katika mpango huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.