Pata taarifa kuu
Rio 2016-HOLLANDE

Michezo ya Olimpiki-2024: François Hollande ziarani Rio

Rais wa Ufaransa François anatazamiwa kufanya ziara mapema asubuhi Alhamisi hii asubuhi, Agosti 4 katika mji wa Rio de Janeiro, nchini Brazil. Rais wa Ufaransa atabaki katika mji huo mpaka sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki (OG) Ijumaa usiku.

François Hollande katika IKulu ya Elysee, Julai 22, 2016.
François Hollande katika IKulu ya Elysee, Julai 22, 2016. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inalenga kuhamasisha wanariadha wa Uaransa lakini pia na hasa kutetea kugombea kwa Ufaransa kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2024.

François Hollande anatarajia kutumia wadhifa wake kwa kutetea Ufaransa kugombea kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki na ile ya wanariadha walemavu ya mwaka 2024. Raisa Hollande atachangia chakula cha jioni na Thomas Bach, Rais wa Kamati ya Olimpiki (IOC) na atafanya mahojiano na watu wengine kadhaa wa taasisi hii ya Olimpiki.

Jitihada hizi za Hollande zinaweza kuwa zenye maamuzi. "Wakati Brazili ilishindia kuwa mwenye wa Michezo ya Olimpiki Septemba 2009, ambapo Rais Lula mwenyewe alikujakutoa ushawishi wake na kukutana na maafisa wa Kamati ya ya Olimpiki (IOC)," amesema mtafiti Pascal Boniface, mwandishi wa kitabu "J.O politique". Rais ambaye anajikita katika Michezo "bado inaendelea kuwa msaada muhimu kwa mafanikio ya operesheni hii".

Kuonyesha kwamba maombi haya ni makubaliano, rais itaonekana sambamba Meya wa Paris Anne Hidalgo na RS Rais wa Ile-de-France, Valérie Pécresse.

Rais wa Ufaransa atakutana na wanariadha wa Ufaransa na maafisa wa Kamati ya Olimpiki (IOC). Kisha Ijuma atakutana na waandishi wa habari kuhusu mpango huo wa michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.