Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RIADHA

Meneja wa timu ya taifa ya riadha ya Kenya, afikishwa Mahakamani

Meneja wa timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa riadha inayoshiriki katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil, Meja Michael Rotich amefikishwa Mahakamani jijini Nairobi.

Michael Rotich akiwasili Mahakamani jijini Nairobi
Michael Rotich akiwasili Mahakamani jijini Nairobi wtop.com
Matangazo ya kibiashara

Rotich, alilazimishwa kurudi nyumbani hata kabla ya wanariadha wake kuanza kushiriki katika michezo hiyo baada ya kudaiwa kuomba rushwa, ili kutoa taarifa mapema kuwasaidia wanariadha kuhusu vipimo vya kubaini ikiwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu mwilini .

Meneja huyo aliyedaiwa kutoa matamshi hayo kwa wanariadha katika kambi ya mazoezi ya Iten mjini Eldoret, alikamatwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi hapo jana.

Upande wa mashtaka umesema unahitaji wiki moja kumaliza uchunguzi dhidi ya Rotich kabla ya kuanza rasmi kwa kesi hiyo, lakini hadi kufikia muda huo, anaendelea kushikiliwa na polisi.

Ripoti la Gazeti la Uingereza la Sunday Times na Televisheni ya Ujerumani ya ARD ilieleza kuwa Meneja huyo alinaswa kwa siri akitaka kulipwa kiasi cha fedha Shilingi Kenya Milioni 1.3.

Mwezi Mei mwaka huu, Shirika la dunia la WADA linalopambana na matumizi ya dawa hizi, liliorodhesha Kenya kama mojawapo ya nchi ambayo haitoi ushirikiano katika vita dhidi ya matumizi ya dawa hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.