Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016

Fahamu timu ya Uganda inayoshiriki michezo ya Olimpiki

Uganda ilishiriki kwa mara ya kwanza katika michezo hii mwaka 1956 lakini ilisusia ile ya mwaka 1976.

Stephen Kiprotich aliposhinda medali ya dhahabu mwaka 2012 jijini London nchini Uingereza
Stephen Kiprotich aliposhinda medali ya dhahabu mwaka 2012 jijini London nchini Uingereza Reuters
Matangazo ya kibiashara

Nchi hii ya Afrika Mashariki katika historia ya michezo hii, imeshinda medali saba katika riadha na masumbwi.

Haijawahi kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

Stephen Kiprotich ndio bingwa mtetezi wa mbio za Marathon kwa upande wa wanaume, taji aliloshinda mwaka 2012 wakati michezo hii ilipofanyika jijini London nchini Uingereza.

Mwanariadha mwingine ambaye anaingia katika vitabu vya historia kushinda medali katika mchezo wa riadha ni John Akii-Bua aliyeshinda mbio za Mita 400 mwaka1972 wakati michezo hii ilipofanyika mjini Munich nchini Ujerumani.

Mwaka huu, Uganda inashiriki katika michezo mitatu riadha, masumbwi na uogeleaji.

Wanamichezo wa kuangaliwa ni pamoja na Stephen Kiprotich, bingwa mtetezi wa mbio za Marathon, Ronald Serugo na Kennedy Katende wote mwanamasubwi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.