Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-UGANDA

Bingwa wa Marathon Stephen Kiprotich apewa makaribisho ya kishujaa jijini Kampala

Stephen Kiprotich, aliyeishindia Uganda medali ya dhahabu katika mbio za Marathon wakati wa michezo  ya Olimpiki jijini London Uingereza amerudi nyumbani na kukaribishwa jijini Kampala na maelfu ya watu kwa mbwembwe vifijo na nderemo.

Daily Moniter
Matangazo ya kibiashara

Kiprotich ambaye ni afisaa wa Magereza amepandishwa cheo na kukabidhiwa hundi la Dola elfu 80 na rais Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebbe .

Rais Museveni ameahidi kumzawadia Dola 400,000 mwanariadha yeyote atakayeishindia nchi hiyo medali katika mashindano yajayo  ya kimataifa.

Aidha Museveni ameahidi kuimarisha viwanja nchini humo na kujenga viwanja vya   wanariadha kufanyia mazoezi yao.

Bingwa huyo wa Olimpiki pia ametoa wito huo kwa serikali ili kuimarisha riadha nchini humo na pia kuwavutia wanariadha chipukizi .

Uganda ilishinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki kwa mara ya mwisho mwaka 1972 kupitia John Akii-Bua katika mbio za mita 400.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.