Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016

Michezo ya olimpiki yasubiriwa kwa hamu kote duniani

Ijumaa ijayo macho na masikio yataelekezwa nchini Brazil, kushuhudia kuanza kwa michezo ya Olimpiki.

Nembo ya michezo ya Olimpiki nchini Brazil 2016
Nembo ya michezo ya Olimpiki nchini Brazil 2016 Reuters/Ricardo Moraes
Matangazo ya kibiashara

Sherehe za ufunguzi zitafanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Maracana jijini Rio de Janeiro.

Haya ni mashindano ya msimu wa joto na yanatarajiwa kumalizika tarehe 21 mwezi ujao.

Wanamichezo zaidi ya 10,000 kutoka mataifa 207 duniani wanatarajiwa kushiriki katika michezo 28.

Mataifa ya Kosovo na Sudan Kusini yatashiriki kwa mara ya kwanza.

Medali 306 zitashindaniwa katika michezo hii na kwa mara ya kwanza, michezo kama raga kwa wachezaji saba kila upande na golf ni miongoni mwa michezo mipya itakayoshudiwa.

Viwanja vitano vitatumiwa katika michezo hii katika miji mbalimbali ambayo ni uwanja wa Amazonia mjini Manaus, uwanja wa Corinthians mjini Sao Paulo, Uwanja wa Fonte Nova mjini Salvador, uwanja wa Nacional Mané mjini Brasilia na ule wa Mineirao mjini Belo Harizonte.

Hii ni michezo ya kwanza msimu wa joyo chini ya rais mpya wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach.

Wanamichezo mbalimbali wameanza kuwasili nchini Brazil kuanza kushiriki katika michezo hii ya kihistoria.

Ukanda wa Afrika Mashariki unawakilishwa pia.

Kenya pia itawakilishwa na timu ya taifa ya mchezo wa raga yenye wachezaji saba kila upande na imepangwa katika kundi moja na New Zealand, Uingereza na Japan.

Kikosi cha Kenya kitafungua michuano hii dhidi ya Uingereza tarehe 9 katika uwanja wa Deodoro mjini Rio de Janeiro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.