Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

FIFA yafichua siri za Jerome Valcke

Waendesha mashitaka wa Uswisi wamethibitisha kwamba shirikisho la Soka Duniani ( FIFA) limekubali kufichua akaunti ya barua pepe ya Jerome Valcke aliyeachishwa kazi kwenye wadhifa wa katibu Mkuu wa FIFA, anayetuhumiwa kuhusika na kashfa ya rushwa.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Jerome Valcke, aliyeachishwa kazi kufuatia tuhuma za ufisadio zinazomkabili. holds up the slip showing "France" during the draw for the 2014 World Cup at the Costa do Sauipe resort in Sao Joao da Mata
Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Jerome Valcke, aliyeachishwa kazi kufuatia tuhuma za ufisadio zinazomkabili. holds up the slip showing "France" during the draw for the 2014 World Cup at the Costa do Sauipe resort in Sao Joao da Mata Reuters/Paulo Whitaker
Matangazo ya kibiashara

Aliachishwa kazi juma lililopita kufuatia madai ya kuhusuka katika mpango wa kuuza tiketi za Kombe la Dunia kwa thamani ya juu.

Wanasheria wa Valcke wamekanusha madai ya mteja wao kuhusika katika kashafa hiyo.

Maafisa wa Uswisi wameanzisha uchunguzi wa rushwa sambamba na Idara moja ya Haki ya Marekani, ambayo ina washitaki maafisa kumi wa soka kwa tuhuma za kasha ya rushwa. Jerome Valkce , raia wa Ufaransa ni kiongozi wa ngazi ya juukatika shirikisho la Soka Duniani (FIFA) anayetuhumiwa kuhusika na kashfa ya rushwa.

Valcke ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huo tangu mwaka 2007 alikanusha hivi karibuni madai hayo na kusema ni mbinu za kumharibia jina baada ya kuonesha nia ya kuwania urais wa Shirikisho hilo.

Tuhma za ufisadi zimekuwa zikiwaumiza viongozi wa soka duniani akiwemo rais wa shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter, ambaye hivi karibuni aliitisha uchaguzi mpya wa Shirikisho hilo mapema mwaka ujao.

Wiki iliyopita viongozi wa mashtaka nchini Uswizi walikubali kuwasafirsuha maafisa 14 wa FIFA wanaoshikiliwa kwenda kufungiliwa mashtaka ya ufisadi nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.