Pata taarifa kuu
FIFA-BLATTER-PLATINI-SOKA

FIFA: Blatter asema Platini amtishia jela ili kumzuia kugombea

Rais wa shirikisho la soka duniani (FIFA) aliyejiuzulu, Joseph Blatter, amesema Jumamosi katika gazeti la kila siku la Uholanzi, Volkskrant, kwamba rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michel Platini alimtishia kufungwa jela iwapo hatoacha kugombea katika urais wa FIFA, mwezi Mei.

Joseph Blatter na Michel Platini, Mei 29 mwaka 2015 katika mkutano mkuu wa FIFA, Zurich.
Joseph Blatter na Michel Platini, Mei 29 mwaka 2015 katika mkutano mkuu wa FIFA, Zurich. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Inasadikiwa kiuwa tishio hili lilitolewa na ndugu ya Sepp Blatter mjini Zurich, masaa kadhaa kabla ya uchaguzi ambao ungempelekea Sepp Blatterkugombea kwa mara nyingine katika uongozi wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Sepp Blatter alisubiri kwa ucahche siku nne ili atangaze kujiuzulu na kurejesha muhula wake kwa ujanja, ikiwa ni mbinu aliotumia kufuatia sakata ya vyombo vya sheria vya Marekani dhidi ya viongozi kadhaa wa FIFA wanaotuhumiwa ufisadi.

" Wakati wa chakula cha mchana, Platini alikaa kwenye meza moja na ndugu yangu (Peter) na kumwambia: mwambie Sepp aachane na kugombeakwenye kiti cha urais wa FIFA, la sihivyo atakwenda jela ", Sepp Blatter amelithibitishia Jumamosi Agosti 15 gazeti la kila siku la Volkskrant, na kuongeza kuwa, maneno hayo yanayokisiwa kutamkwa na Platini aliayapata hivi karibuni akiyaambiwa na nduguye.

Jumamosi mbele ya shirika la habari la Ufaransa (AFP), chanzo kilio karibu na Michel Platini kimeelezea kauli hii mpya ya Sepp Blatter kuwa ya " uzushi ". Hii ni moja ya "mfululizo wa majaribio ya Zurich yaliokua yakiandaliwa ili kupelekea watu wanasahau matatizo yanayolikabili shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ", chanzo hicho kimeendelea, kikisema kuwa "rais wa UEFA hawezi kujieleza kuhusu madai hayo yasio kuwa na msingi ".

" Michel Platini kwa sasa anaangilia jinsi gani kutakuewpo na maandalizi ya mpango ambao utaweza kurejesha sura mpya na sifa za FIFA na ambao utaweza hasa kuendeleza soka duniani kote", chanzo hicho kimesisitiza kuhusu rais wa UEFA, ambaye ni mgombea rasmi wa urais wa FIFA tangu Julai 29.

Uchaguzi huo utafanyika Februari 26 mwaka 2016 mjini Zurich. Mgombea mwengine anaye julikana rasmi wakati huu ni Chung Mong-Joon, kutoka Korea Kusini, ambaye anatazamiwa kutangaza kwa kina mpango wake Jumatatu mjini Paris. Mwanamfalme wa Jordan, Ali bin Al Hussein, ambaye alikua mgombea pekee dhidi Blatter mwezi Mei, pia anaweza kuingia katika kinya'nganyiro hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.