Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA-MICHEZO

ACN 2015: Angola, Misri, Gabon Nigeria zakataa

Mashirikisho ya soka katika nchi za Misri, Gabon, Nigeria yamekataa kuanda michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015, ambayo imepangwa kuchezwa tangu mwezi wa January mwaka 2015.

Wakati wa mchuano kati ya Sudani na Afrika Kusini katika kufuzu kwa CAN 2015.
Wakati wa mchuano kati ya Sudani na Afrika Kusini katika kufuzu kwa CAN 2015. AFP PHOTO / EBRAHIM HAMID
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka Afrika CAF, limekua likijaribu kuokoa jahazi baada ya Morocco, ambayo ingelikua mwenyeji wa michuano hiyo kukataa ikihofia mambukizi ya virusi vya Ebola.

Awali Morocco iliomba michuano hiyo iahirishwe hadi mwaka 2016, lakini shrikisho la soka Afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA, vilipinga hoja hiyo. Hata hivo CAF ilifahamisha hivi karibuni kwamba nchi zaidi ya kumi ziko kupokea michuano. Nchi moja baada ya nyinge zimeanza kubadili msimamo wao kufuatia hofu ya kuambukizwa raia wao virusi vya Ebola.

Miezi miwili imesalia ili michuano hiyo ianze. Novemba 14 au 15 CAF inatazamiwa kutangaza jina au majina ya mataifa yatayojikubalisha kusimamia maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Baadhi ya mataifa yaliyokua yamepewa nafasi kubwa ya kuandaa michuano hiyo baada ya Morocco kujiondoa, yamebaini kwamba hayako tayari kusimamia maandalizi ya michuano hiyo.

Angola, Gabon, Nigeria, Misri, zimejiondoa katika kinyanganiro hicho. CAF ilikua na imani na Qatar kuanda michuano hiyo lakini katika dakika za mwisho Qatar imekataa. Iwapo Qatar ingelikubali kusimamia maandalizi ya michuano hiyo, ingelikua ni kwa mara ya kwanza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kuchezwa nje ya Afrika.

 Hii hapa ni ratiba ya michuano tangu Novemba 14 hadi 19 mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.