Pata taarifa kuu
FIFA-Soka-michezo

Ebola: Fifa yaunga mkono CAN 2015 kuchezwa Morocco

Fifa imechapisha "mapendekezo" kadhaa juu ya kudhibiti mlipuko wa Homa ya Ebola. Kwa mujibu wa shirikisho hilo linalosimamia soka duniani, michuano ya kombe la dunia la vilabu inayoandaliwa Morocco hayiko hatarini.

Uwanja Mohammed-V wa Casablanca, Morocco.
Uwanja Mohammed-V wa Casablanca, Morocco. AFP PHOTO / STR
Matangazo ya kibiashara

Hata hivo Fifa imeunga mkono uamzi wa Shirikisho la Soka Afrika CAF ambao umezitaka mechi inayohusisha moja ya mataifa yanayo athirika kuchezwa katika nchi ambayo haijaathirika.

Fifa imechapisha Jumanne Oktoba 28 mapendekezo kuhusu namna ya kudhibiti Homa ya Ebola, huku ikibaini kwamba maandalizi kuhusu kombe la dunia la vilabu yanaendelea vizuri “kama ilivyopangwa”.

Fifa ambayo imebaini kwamba imekua ikiwasiliana mara kwa mara na Shirika la afya duniani WHO ili kujifunza madhara ya virusi kwa afya ya umma duniani kote, mikusanyiko hasa athari zake kwa soka, imesema inaunga mkono uamzi wa Shirikisho la soka Afrika wa kuendelea na maandalizi ya kombe hilo.

Shikisho hilo la kimataifa limeshauri mashabiki wa vilabu mbali mbali kuhamasishwa kuhusu namna ya kujilinda na virusi vya Ebola.Michuano ya kombe la dunia la vilabu itachezwa Morocco kuanzia Desemba 10 hadi 20 mwaka 2014.

Morocco iliomba Oktoba 10 kuahirisha michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2015 kwa kuhofia maambukizi ya Ebola, wakati ambapo Shirikisho la soka Afrika CAF lilifahamisha siku moja baadaye kwamba ratiba ya michuano hiyo haitobadilishwa. Michuano hiyo imepangwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015 nchini Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.