Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA-MICHEZO

Michuano ya CAN 2015 itachezwa Januari 17 hadi februari 8 mwaka 2015

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza Jumatatu Novemba 3 kwamba michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika itachezwa kama ilivyopangwa Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015.

Mchezaji wa Nigeria, Elderson Echiejile akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao dhidi ya Mali katika nusu fainali ya michuanao ya Kombe la mataifa barani Afrika, Februari 6 Durban.
Mchezaji wa Nigeria, Elderson Echiejile akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao dhidi ya Mali katika nusu fainali ya michuanao ya Kombe la mataifa barani Afrika, Februari 6 Durban. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo shirikisho hilo limeipa muda Morocco ili iwe imekwisha chukua msimamo

hadi Novemba 8. Morocco iliomba hivi karibuni michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika iahirishwe ikihofia mambukizi ya virusi vya Ebola kwa wachezaji na watu watakao kuwa wamekuja kuhuzuria michuano hiyo.

CAF hatimaye imeamua rasmi kachia michuano hiyo ichezwe katika muda uliyopangwa. Michuano hiyo itaanza kuchezwa Januari 17 hadi Februari 8. Hadi sasa haijajulikana ni nchi gani itakubali kupokea michuano hiyo ya Kombe la mataifa ya Afrika.

" Kamati ya Utendaji ya CAF imeitaka Morocco kufafanua msimamo wake wa mwisho kabla ya Novemba 8, 2014", Shirika la soka barani Afrika imeandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijami wa twitter. Mkutano wa shirikisho la soka barani Afrika umepangwa kufanyika Novemba 11 katika mji mkuu wa Cairo Misri, ili "kuchukua umzi unaohitajika".

Kamati kuu ya Shirikisho la soka barani Afrika ilizungumzia suala hilo wakati wa mkutano wa wajumbe wa kamati hiyo uliyofanyika Jumapili Novemba 2 katika mji mkuu wa Algeria Algiers.

Morocco iko tayari kupokea michuano hiyo lakini hapana mwezi Januari. Kufuatia mapendekezo ya Shirika la afya duniani (WHO), Morocco imekua na hofu ya mambukizi ya virusi vya Ebola kwa wachezaji na watu ambao watakua wamekuja kuhuzuria michuano hiyo.
Baadhi ya wachezaji nyota kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wamekua wakiunga mkono uamzi wa Morocco wa kuahirishwa kwa michuano hiyo kufuatia mlipuko wa Ebola ukianzia kwa kipa wa Nigeria Vicent Enyeama.

" Michuano ya CAN 2015 haipaswi kuchezwa muda huo uliopangwa. Siyo uamuzi wangu, lakini nadhani ni hatari kwa kila mtu. Katika utamaduni na mila za kiafrika, watu siku zote wanataka wagusane kwa kusabahiyana. Lakini sasa, mimi si CAF, na wala sina uamzi wowote. Hata hivyo, kama uamzi utachukuliwa wa kucheza michuano hiyo nchini Morocco kwa tarehe iliyopangwa, mimi ntakuepo”, amesema Enyeama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.