Pata taarifa kuu

WHO: Syria yakabiliwa na hatari ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu

Haya ni madhara mengine ya ukame katika Mashariki ya Kati, Syria inahofia kurejea kwa ugonjwa wa kipindupindu. Shirika la Afya Duniani lilionya siku ya Jumanne Septemba 13 juu ya hatari kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo. Nchi jirani ya Iraq tayari imeathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu tangu mwanzoni mwa majira ya kiangazi.

Kambi ya Wasyria waliohamishwa kutoka mkoa wa Idleb huko Aleppo, karibu na mji wa Maaret Misrin, kaskazini magharibi mwa Syria, tarehe 11 Julai 2020.
Kambi ya Wasyria waliohamishwa kutoka mkoa wa Idleb huko Aleppo, karibu na mji wa Maaret Misrin, kaskazini magharibi mwa Syria, tarehe 11 Julai 2020. OMAR HAJ KADOUR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchini Syria, majimbo yaliyoathiriwa zaidi ni Aleppo kaskazini na Raqqa na Deir Ezzor kaskazini mashariki, chini ya udhibiti wa Wakurdi. Huko Deir Eizzor, ugonjwa huo unasemekana kuenea kupitia maji machafu ya kunywa, kulingana na Shirika la Haki za Kibinadamu nchini Syria. Mamlaka inaripotiwa kusitisha kusambaza klorini kwa vituo vya kusukuma maji miezi mitatu iliyopita.

Jumla ya vifo vitano na makumi ya kesi tayari yamerekodiwa. Ugonjwa huo ulikuwa haujasambaa nchini Syria tangu mwaka wa 2009.

Kipindupindu ni maambukizo ya kuhara ya papo hapo ambayo wakati mwingine husababisha upungufu wa maji mwilini. Yanaambukizwa kwa njia ya maji au chakula.

Tishio halisi la kikanda

Tayari mwathirika wa ukame unaosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko katika mkondo wa Euphrates, baada ya miaka kumi na moja ya vita, Syria inakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ya kunywa. Kabla ya 2010, 98% ya wakaazi wa jiji na 92% ya wakaazi wa vijijini walikuwa na maji safi. Lakini mzozo umeharibu karibu theluthi mbili ya mitambo ya kusafisha maji, nusu ya vituo vya kusukuma maji na theluthi moja ya mitambo ya maji, kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ya mwezi wa Aprili.

Siku ya Jumatatu, Umoja wa Mataifa ulihimiza nchi wafadhili kutoa haraka fedha za ziada ili kupambana na mlipuko huo. "Hii ni tishio kubwa kwa Syria na kanda nzima," alisema mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Imran Riza.

Inakadiriwa kuwa kuna visa kati ya milioni 1.3 na milioni 4 vya kipindupindu duniani kote kila mwaka, na kusababisha vifo kati ya 21,000 na 143,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.