Pata taarifa kuu

Syria: Iran yakabiliwa na mashitaka mbele ya ICC kwa 'uhalifu dhidi ya binadamu'

Malalamiko hayo yaliwasilishwa siku ya Jumatano, Februari 16 kwa mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Iran kwa jukumu lake nchini Syria. Katika 'malalamiko' hayo pia wanalaani uhalifu wa utawala wa Bashar el-Assad. Mwendesha mashtaka hana muda wa kujibu.

Mlango wa mahakama ya jinai ya ICC huko  Hague nchini Uholanzi.
Mlango wa mahakama ya jinai ya ICC huko Hague nchini Uholanzi. REUTERS/Jerry Lampen/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa Iran kulengwa na "malalamiko" yaliyowasilishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Shirika lisilo la kiserikali la Haki za Binadamu nchini Iran (IHRDC), shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Marekani, linashutumu, katika hati iliyotumwa kwa mwendesha mashtaka wa Mahakama Jumatano hii, uhalifu dhidi ya binadamu unaofanywa na Iran na Walinzi wa Mapinduzi nchini Syria. .

"Malalamiko" yaliyoelekezwa kwa Karim Khan yamejikita hasa juu ya ushuhuda wa waathiriwa wa Syria ambao wamekimbilia nchini Jordan. Miongoni mwao, waandishi wa habari, wanaharakati, na jumuiya za miji na vijiji wanakoishi Waislamu kutoka dhehebu la Sunni wanaochukuliwa kuwa wapinzani na utawala wa Bashar el-Assad na hasa wanaolengwa na majeshi ya Iran na Syria.

Mamlaka yenye mipaka

Ikiwa mwendesha mashtaka ataamua kuchukua kesi hiyo, huenda akachunguza tu sehemu ndogo ya uhalifu. Iran wala Syria ni nchi ambazo hazijajiunga na ICC, lakini uhalifu unaofanywa kwa pamoja kati ya majeshi ya Syria na Iran umewalazimu watu kukimbia na kukimbilia Jordan, ambayo ini mwanachama wa Mahakama hiyo tangu mwaka 2002. "Ushahidi unaonyesha kuwa raia wa Syria wamekumbwa na uhalifu dhidi ya binadamu kwa kufukuzwa na kuteswa, amebaini mwanasheria wa shirika hilo, Haydee Dijkstal, na baadhi ya uhalifu huu ulifanyika katika nchi ya Jordan. "

Kwa hivyo shirika hilo linaona kuwa mahakama hiyo ina uwezo wa kuchunguza uhalifu unaofanywa dhidi ya watu wa Syria waliolazimika kukimbilia nchini Jordan. Mnamo mwaka wa 2019, ofisi ya mwendesha mashtaka, kwa msingi sawa wa kisheria, ilifungua uchunguzi juu ya uhalifu uliofanywa dhidi ya wakimbizi wa Rohingya huko Bangladesh.

Wanamgambo wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran

Kwa mujibu wa shirika hilo, "vikosi vinavyoongozwa au kuungwa mkono na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimehusika katika mapigano kote Syria na vimekuwa na uwepo mkubwa katika mapigano kusini mwa Syria, ambayo yamesababisha kuhamishwa kwa maelfu ya Wasyria waliokimbia ghasia hadi Jordan."

IHRDC inalaani msaada wa kifedha, kijeshi na teknolojia wa Iran kwa vikundi vya wanamgambo wa Kihia wanaofanya kazi nchini Syria. Shirika hilo linadai kwamba Walinzi wa Mapinduzi waliwafunza wanamgambo wa kijeshi wa Syria, na "walituma maelfu ya wanajeshi wa Iran na vikundi vya wanamgambo wa Kishia" wakiwemo Hezbollah ya Lebanon na wanamgambo wa Afghanistan Liwa Fatemiyoun.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.