Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Urusi: Wanajeshi 92 wa Ukraine wahukumiwa kwa kuhusika na uhalifu wa kibindamu

Kamati ya uchunguzi ya Urusi imesema kuwa imewahukumu wanajeshi 92 wa Ukraine baada ya kuwakuta na makosa ya uhalifu wa kibinadamu.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na wakuu wa jeshi la nchi yake
Rais wa Urusi Vladimir Putin na wakuu wa jeshi la nchi yake AP - Alexei Nikolsky
Matangazo ya kibiashara

Mchunguzi mkuu wa kamati hiyo ya Urusi ,Alexander Bastrykin ,katika taarifa yake kwa mtandao wa habari unaomilikiwa na serikali wa Rossiiskaya Gazeta ,amesema kuwa zaidi ya visa  1,300 vinavohusishwa na uhalifu vimeanza kuchunguzwa.

Kiongozi huyo aidha amependekeza kuundwa kwa tume ya kimataifa inayojumuisha nchi za Iran, Syria na Bolivia –nchi ambazo ni washirika wa Urusi.

Haya yanajiri wakati huu ambapo pia Ukraine na yeneyewe ikiwa inafanya uchunguzi wake kuhusu makosa ya uhalifu wa kibinadamu inayosema yanatekelewa na Moscow.

Licha ya 92 hao kuhukumiwa, Bastrykin, ameeleza kuwa watu wengine 96 wakiwemo makamanda wa jeshi 51 wa Ukraine wanatafutwa na Urusi.

Ukraine, mapema mwezi huu ilisema inachunguza zaidi ya visa 21,000 vya uhalifu wa kibinadamu ambavyo vimetekelezwa na wanajeshi wa Urusi tangu Urusi ilipoivamia Kyiv mwezi Februari.

Mwezi Mei, Ukriane ilimfunga jela maisha kamanda wa jeshi la Urusi baada ya kumkuta na makosa ya kumuuwa raia wake.

Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu wa Jinai ICC,tayari imewatuma maofisa na wataalam wake wa uchunguzi nchini Ukraine.

Kremlin kwa upande wake imeendelea kukana madai kuwa inawalenga raia katika mapambano yake na wanajeshi wa Ukraine. Badala yake imeituhumu Ukraine kwa kuwauwa raia wake –madai ambayo yamekashifiwa na viongozi wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.