Pata taarifa kuu
IRAQ-USALAMA

Iraq: Waziri Mkuu anusurika jaribio la mauaji

Nchini Iraq, Waziri Mkuu Mustafa Al-Kadhimi amenusurika jaribio la mauaji usiku wa Novemba 6 kuamkia 7. Ndege isiyo na rubani iliyonasa ililenga makazi yake katikati mwa mji mkuu wa Iraq. Waziri Mkuu hakujeruhiwa, lakini Iraq sasa inaonekana kuwa kwenye sintofahamu.

Vikosi vya usalama vya Iraq nje ya Eneo la Kijani la Baghdad, Novemba 7, 2021.
Vikosi vya usalama vya Iraq nje ya Eneo la Kijani la Baghdad, Novemba 7, 2021. AFP - SABAH ARAR
Matangazo ya kibiashara

Raia wengi wa Iraq waliamshwa usiku wa manane Jumapili hii na mlipuko mkali, uliofuatiwa na milio mingi ya risasi, kuelekea kituo cha kisiasa na kidiplomasia cha mji mkuu wa Iraq, ameripoti mwandishi wetu huko Baghdad, Lucile Wassermann. Shambulizi, lililotekelezwa na ndege isiyo na rubani iliyotegwa mabomu, dhidi ya makazi ya Waziri Mkuu wa Iraq, katikati ya Ukanda wa Kijani, wilaya yenye usalama wa hali ya juu ambapo ni makao makuu ya taasisi za kisiasa.

Jaribio la mauaji lilitekelezwa na "ndege tatu zisizo na rubani, mbili kati yazo zilidunguliwa" na mlinzi wa karibu wa Moustafa Al-Kadhimi, kulingana na vyanzo viwili vya usalama. Vifaa hivyo vitatu "vilizinduliwa kutoka eneo lililo karibu na Daraja la jamhuri", kabla ya kuelekea Eneo la Kijani, kimesema moja ya vyanzo hivi, kikibainisha kuwa "ndege mbili zisizo na rubani zilidunguliwa" zikiwa angani. Ndege ya tatu iliweza kutekeleza shambulio la bomu dhidi ya nyumba ya Waziri Mkuu ambaye hakujeruhiwa, lakini walinzi wawili walijeruhiwa.

Saa chache baadaye, Mustafa Al-Kadhimi alizungumza na kusema kwamba yko salama, na hasa kutoa wito wa utulivu katika mji mkuu. Macho yote sasa yanaelekezwa kwa wanamgambo wanaoiunga mkono Iran, wakiwa na hasira kwa wiki kadhaa kwa sababu mrengo wao wa kisiasa ulipoteza viti vingi katika Bunge wakati wa uchaguzi uliopita wa wabunge.

Mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni, wamemtishia mkuu wa nchi wa Iraq. Shambulio hilo halijadaiwa lakini sasa linaipeleka Iraq kwenye sintofahamu, ambapo hali ya usalama inaweza kuwa mbaya wakati wowote.

Marekani mara moja imeshutumu "kitendo kilichowazi cha kigaidi" dhidi ya Waziri Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.